TANGAZO


Tuesday, October 28, 2014

Wagoma wakitaka marufuku kuondolewa Lamu

Lamu Curview
Wafanyibiashara na wakaazi wa Lamu kusini mwa Kenya wamefanya mgomo kuhusu kuongezwa kwa mda wa marufuku ya kutotoka nje kutoka saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi iliowekwa na serikali miezi minne iliopita.
Maduka yote kufikia sasa yamefungwa katika kisiwa cha lamu .
Ndege zinazotoka na kuingia katika uwanja wa ndege wa Manda hatahivyo hazikuathiriwa na mgomo huo.
Lakini uchukuzi kwa njia ya majini umeathiriwa kwa kuwa wafanyikazi wanaoendesha mashua za uchukuzi wamekataa kufanya kazi.
Hakuna ghasia zilizoripotiwa kufikia sasa na maafisa wa polisi wameongeza uwepo wao mjini humo.
Huku marufuku hiyo ikiendelea kuheshimiwa katika kaunti yote ya Lamu,na hivyobasi kuathiri usafiri wa watu na mali,katika kisiwa cha Lamu marufuku hiyo inaanza kuheshimiwa kuanzia saa tatu.
Kiongozi wa Upinzani nchini kenya Raila Amollo Odinga ametoa wito wa kuondolewa kwa marufuku hiyo akisema kuwa imewakandamiza raia wa Lamu na kuathiri uchumi wao.Vilevile Viongozi wa kiislamu pia wametoa wito wa marufuku hiyo kuondolewa.
Shirika la mawakili nchini kenya LSK pia limetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mkuu wa Polisi David Kimaiyo kuhusu kile wanachoona kama masharti yasio ya kisheria.
Hatahivyo baadhi ya madiwani na mbunge mmoja wanaamini kwamba marufuku hiyo inahitajika kwa kuwa usalama wa eneo hilo bado haujaimarika.

No comments:

Post a Comment