Pengo lililopo kati ya wanaume na wanawake linaendelea kuzibika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni,kutokana na hatua za baadhi ya wanawake kuingia katika ulingi wa siasa pamoja na kufanya kazi.
Kulingana na jukwaa la kiuchumi duniani WEF hatua hiyo imeshinikizwa na maswala ya kiuchumi,kisiasa na kielimu katika mataifa 142.
Tangu ripoti hiyo ianze miaka tisa iliopita ,takriban mataifa 105 yamepunguza taofauti yao ya kijinsia huku mataifa matano yakisalia na pengo kubwa.
Taifa la Iceland ndio linaloongoza kwa mwaka wa sita huku Yemen ikisalia kuwa ya mwisho.
Mataifa ya Scandinavia ndio yanayoongoza huku Finland,Norway na Sweden yakifuatia nyuma ya Iceland katika mataifa matano bora.
Mataifa yote yamasheherekea kile walichokitaja kama maendeleo yao ya kisiasa.
Uingereza imeshuka nafasi nane chini katika orodha hiyo na kuwa ya 26,huku Rwanda ikipanda hadi nafasi ya saba kutoka mataifa 20 bora na kuifanya kuwa taifa lwa kwanza barani Afrika.
Kulingana na Jukwaa hilo la kiuchumi ,mabadiliko kuhusu mapato ya wanawake ndio sababu kuu ya kushuka kwa Uingereza.
Upande mwengine wa Atlantic ,Marekani imepanda nafasi tatu na kuwa nambari 20 kwa kuwa tofauti ya mishahara kati ya wanawake na wanaume imepungua huku idadi ya wabunge wanawake na wale walio na nyadhfa za uwaziri zikiongezeka.
Kulingana na mwandishi wa ripoti hiyo Saadia Zahid ,mafanikio ya Rwanda yanatokana na kwamba kuna wanawake wengi sawa na wanaume wanaofanya kazi nchini humo,huku wanawake wengi pia wakifanya kazi katika wizara mbalimbali badala ya kuimarishwa kwa idara za afya na huduma za elimu.
Mataifa mengine yalioshangaza wengi katika orodha hiyo ni pamoja na Nicaragua ,ambalo limepanda hadi nafasi ya sita kutoka nafasi ya 10 na Ufilipino ambalo ndio taifa bora kutoka bara Asia likiwa nafasi ya tisa.
No comments:
Post a Comment