Polisi hawatachukua hatua zaidi dhidi ya mshambuliaji wa timu ya Liverpool Mario Baloteli kuhusiana na madai kwamba mchezaji huyo alitumia maneno machafu dhidi ya mwanamke mmoja aliyekua akichukua picha za gari lake.
Balotelli anadaiwa kumkaribia msichana wa mwanamke huyo ambaye alikuwa akichukua picha za gari hilo aina ya ferrari.
Hatahivyo mwanamke huyo ameamua kutowasilisha ombi la malalamishi yake.
''Hakuna uhalifu wowote uliotolewa ama kurekodiwa'' ilisema taarifa ya polisi kutoka Manchester.
Maafisa wa polisi waliitwa katika barabara ya Pewsey,Wythenshawe,mda mchache tu baada ya saa tisa jioni siku ya alhamisi kufuatia ripoti za tabia za kutishia.
''Maafisa wa polisi wamezungumza na mlalamisi na hakuna hatua zaidi zitakazochukuliwa''ilisema ripoti hiyo
Tukio hilo lilifanyika siku ambayo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alibadilishwa wakati wa mapumziko wakati ambapo timu hiyo ilikuwa iko chini ya mabao matatu kwa bila dhidi ya Real madrid wiki iliopita.
No comments:
Post a Comment