TANGAZO


Tuesday, October 14, 2014

Wafanyakazi wa Tigo washiriki matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salaam

1 (3) 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akifanya mazoezi kabla ya kuanza matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam leo, Matembezi hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo.
3 (1) 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid akisalimiana na Meneja wa huduma za Jamii wa kampuni ya simu yaTigo, Woinde Shisael (kulia) kabla ya kuanza kwa matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam leo, yaliyodhaminiwa na Kampuni hiyo. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Diwani Msemwa (kushoto kwake) na Mkurugenzi wa Wellworth Tanzania, Saul Basckin.
5 (2) 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid (watatu kushoto) akiongoza matembezi ya kuchangia fedha kwa ajili ya Saratani ya matiti jijini Dar es Salam leo, yaliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo. Kulia ni Meneja wa huduma za Jamii wa Kampuni ya simu ya Tigo, Woinde Shisael na kushoto kwa waziri ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Diwani Msemwa.
7
Meneja wa Huduma za Jamii wa Kampuni ya Simu yaTigo, Woinde Shisael, akizungumza, wakati wa hafla hiyo. 

No comments:

Post a Comment