Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa katika jiwe la msingi
wakati wa uzinduzi wa kijiji cha mfano cha vijana Pathfinders Green City
katika kata ya Igigwa wilayani Sikonge leo.Rais Kikwete yupo Mkoani
Tabora kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kukagua na kuzindua miradi ya
maendeleo ambapo pia atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha mbio za
mwenge hapo kesho.watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bi.Fatma
Mwassa na wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Bi. Hanifa Selenga.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya uchakataji asali kutoka
kwa mmoja wa vijana waishio katika kijiji cha mfano cha vijana
wajasiriamali katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge, Mkoani Tabora
leo.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua baadhi ya madawati yaliyotengenezwa
na kikundi cha vijana wajasiriamali katika kijiji cha mfano cha
Pathfinders katika kata ya Igigwa, wilayani Sikonge,Mkoani Tabora muda
mfupi baada ya kukizindua kijiji hicho.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na
vijana wajasiriamali katika kijiji hicho cha mfano. (Picha zote na Freddy
Maro)
No comments:
Post a Comment