*Wateja kufurahia ubora wa juu wa huduma kutoka Airtel mjini Zanzibar
Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar, Abdallah Mwinyi akijiandaa kukata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la Huduma kwa Wateja la Airtel jijini Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba na kulia ni Maneja wa Kanda ya Zanzibar, Mariam Yussuf.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kushoto), akimwelekeza jambo mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa Zanzibar, Abdallah Mwinyi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa duka la huduma kwa Wateja kisiwani Zanzibar ,wakishuhudiwa na wageni wengine waalikwa.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kushoto), akimwelekeza mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib, Zanzibar, Abdallah Mwinyi jinsi huduma ya Airtel money ilivyoboreshwa wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa duka la huduma kwa Wateja kisiwani Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar, Abdallah Mwinyi akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa duka la huduma kwa wateja la Airtel jijini Zanzibar. Akifuatiwa na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba na Maneja wa Kanda ya Zanzibar Mariam Yussuf.
Na Mwandishi wetu, ZanzibarAIRTEL Tanzania imefungua duka lake la kisasa kisiwani Zanzibar lililopo mtaa wa Mlandege lenye uwezo wa kuhudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku.
Ni duka la kisasa ambalo lipo karibu na wateja lenye kurahisisha maisha ya wateja wote wa Airtel kisiwani Zanzibar.
Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo Mkurugenzi kwa huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba alisema, "kwamba kupanua kwetu kwa huduma za mtandao kwa wateja wetu ni ishara tosha ya kuonyesha ni jinsi gani Airtel inajali wateja wake na kuwapatia wateja wetu huduma bora na za kibunifu.
"Ni juhudi zetu na mafanikio yetu ya kuwa na wateja zaidi ya milioni 9 tulionao ndio yanayotufanya tuweze kuwashukuru wateja wetu kwa kuwapatia huduma nzuri zenye Kiwango cha juu. Kwa huduma tunazozitoa kupitia maduka yetu yaliyoenea hapa nchini maduka haya yanauwezo wa kutoa huduma zenye kiwango cha juu yanayotoa huduma kwa masaa mengi na kutoa huduma nzuri kwa wateja.
Uzinduzi wa maduka yetu ni mafanikio makubwa kwetu na hii ni shukurani yetu kwao kwa kuwaonyesha ni jinsi gani tunawajali wateja wetu.
Hafla hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa Abdallah Mwinyi, ambaye aliipongeza Airtel kwa ajili ya kuleta huduma zake karibu na watu wa Zanzibar.
"Mbali na kutatua matatizo ya wateja, mtazamo huu mpya wa duka hili ni maendeleo tosha kwa wakazi wa Zanzibar kwani huduma zinazotolewa hapa ni za kiwango kizuri na uwezo mkubwa ambapo wateja wa Airtel wamekuwa wakihitaji hapa kisiwani Zanzibar. alisema.
Mwinyi alisema kuwa, huduma mbalimbali za mawasiliano zinazotolewa na Airtel kuanzia , ujumbe, Inteneti , usajili, huduma za Airtel Money ambazo zinarahisisha maisha ya wananchi katika jamii. "Huduma hizi zinaleta matokeo mazuri katika namna ya kufanya biashara na kuboresha maisha ya maelfu ya wakazi wa Zanzibar na mamilioni ya Watanzania kwa ujumla," aliongeza Mwinyi.
Kama sehemu ya huduma nzuri , Airtel tayari imekarabati maduka mengine katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Bukoba, Mbeya, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Tabora na leo hapa Zanzibar.
Maduka ya Airtel yataendelea kutoa huduma mbali mbali zenye kiwango cha juu na upatikanaji wa bidhaa zake kama vile modems, simu, malipo ya bili,huduma za Airtel money na huduma nyingine nyingi.
Tumewekeza kwa kiwango kikubwa katika mtandao wetu ili kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma sahihi na ya kiwango cha juu.
No comments:
Post a Comment