Bw.
Japhet Kwangula akieleza katika Mkutano wa wakulima wa pamba uliofanyika hivi
karibuni wilayani Bunda juu ya umuhimu wa kupata pembejeo kwa wakati na kwa kiwango
kinachotakiwa. Katika mkutano huo, wakulima waliweza kupata fursa ya kujadili
ya mafanikio na changamoto zilizopo kwenye sekta ya pamba sambamba na
kujadiliana namna ya kupata njia sahihi ya kuwawezesha kufanya vizuri na hivyo
kufikia malengo kwa msimu ujao.
Mmoja
ya wakulima wa pamba akichangia katika majadiliano juu ya faida ya kilimo cha
mkataba kwenye mkutano wa wakulima wa pamba uliokuwa ukichambua juu ya
mafanikio, changamoto na njia sahihi za kuweza kufanya sekta hiyo kuendeshwa
kwa mafanikio zaidi kwa msimu ujao. Mkutano huo ulifanyika wilayani Bunda hivi
karibuni.
Katibu
Tawala wa Wilaya ya Bunda, Bw. Dominicas Lusasi akiongea na wakulima wa wilaya
hiyo kwenye majadiliano yaliyolenga kuwapa wakulima wa Bunda motisha kwa kuwa na pamba yenye ubora wa hali
ya juu. Mkutano huo wa wakulima wa pamba ulifanyika hivi karibuni wilayani
Bunda. Mkutano huo uliwapa fursa wakulima ya
kujadili ya mafanikio na changamoto katika sekta ya pamba sambamba na
kujadiliana njia bora ya kuwezesha kufanya vizuri na kufikia malengo kwa msimu
ujao.
No comments:
Post a Comment