Mgogoro kuhusu mkufunzi halisi atakayesimamia timu ya taifa la Sierra Leone umezuka huku shirikisho la soka nchini humo SLFA na wizara ya michezo zikiwachagua makocha wawili tofauti watakaosimamia mechi ya kufuzu katika michuano yua bara Afrika kati ya taifa hilo na Cameroon.
Hatua hiyo imeathiri maandalizi ya mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa mjini Younde mnamo tarehe 11 Octoba na 15 Octoba.
Shirikisho la soka nchini Sierra leone limemchagua John Ajina Sesay kama kaimu kocha.Atasaidiwa na Abdulai Bah.
Uteuzi huo unajiri siku kumi na sita baada ya kocha mwengine Atto Mensah kuchaguliwa kama mkufunzi wa timu hiyo na wizara ya Michezo ili kuchukua mahala pa Jonathan Mckinstry.
Aliyekuwa mchezaji wa Sierra Leone John Sama alitajwa kama naibu wa Mensah.
Mensah tayari amekitaja kikosi chake kwa mechi hizo mbili.
Lakini mkuu wa mauzo na habari katika Shirikisho hilo la soka Abu Bakarr Kamara amesema kuwa wamemchagua kocha mpya kwa kuwa hakufuzu kujaza wadhfa huo.
No comments:
Post a Comment