Mkurugenzi wa Ubunifu wa Kampuni ya GODTEC Bw. Aloyce Midelo akielezea namna Kampuni yao inavyosaidia vijana katika kujiari kwa kuanzisha makampuni yao wenyewe. ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akifafanua namna NHC ilivyo saidia vijana kupitia mradi wa ufyatuaji wa matofali na ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi
Baadhi ya Maafisa Vijana wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji (hawapo pichani)
Baadhi ya Maafisa Vijana wakifuatilia mada
mbalimbali kutoka kwa wawezeshaji (hawapo pichani) leo. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
Na
Jonas Kamaleki
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Bi Sihaba Nkinga amewataka vijana kujitambua na kuwa na mtazamao
chanya ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Haya yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga katika Kikao kazi cha Maafisa vijana kutoka
nchi nzima kilichofanyika mjini Tabora.
Bibi. Sihaba amesema Vijana wawe wabunifu na kuibua
miradi mbali mbali ili waweze kupata msaada wa Serikali katika kuendesha miradi
yaona kuwataka waache tabia ya mazoe na badala yake wachape kazi.
“Kuweni wabunifu wa programu mbali mbali kuwasaidia
vijana ili waondokane na malalamiko yakila siku ktoka kwa Vijana yatokanayo na
ukosefu wa ajira,” Alisema Bi Sihaba.
Aidha Katibu
Mkuu huyo aliwahakikishia vijana kuwa upo Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ambao
kazi yake ni kuwawezesha vijana kuendeleza miradi yao kwa njia ya mkopo wenye
riba nafuu.
Aliongeza kuwa ni vyema Halmashauri zote nchi kutii
waraka unaowataka kutenga asilimia tano ya mapato kwa ajili ya Maendeleo ya
Vijana kwani kwa kufanya hivyo kunapunguza changamoto zinazowakabili baadhi ya
Maafisa Vijana nchini.
Bibi. Sihaba aliongeza kuwa vijana wajiunge kwenye vikundi na kushirikiana
na viongozi wao katika ngazi za Mikoa na Wilaya ambao nao wana program
mbalimbali za kusaidia vijana.
“Ikumbukwe kuwa baadhi ya mikoa imeshaanza kutenga
fedha kwa ajili ya maendeleo ya vijana. Mfano mkoa wa Tabora umetenga shilingi
bilioni 1.8 kwa ajili ya maendeleo ya vijana”.Alisema Bibi Sihaba.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Vijana, Bwana James Kajugusi amewataka vijana wakabiliane na changamoto
zilizopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Kajugusi alitumia wasaa huo kuwakumbusha maafisa
Vijana kote nchini kutekeleza majukumu yao na kuwahakikishia kwamba Serikali
inaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabi katika kufanikisha utendaji
wao.
Moja ya jukumu la Msingi la Afisa Vijana ni pamoja
na kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu
maendeleo ya vijana hasa katika maeneo ya vita dhidi ya UKIMWI, madawa ya
kulevya, uchumi na uzalishaji mali na masoko.
No comments:
Post a Comment