Timu ya Ikulu ya kuvuta kamba wanaume wakiwa kwenye mechi za hatua ya timu 32 wakiwavuta timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwashinda kwa 2-0 wakati wa mashindano ya SHIMIWI taifa leo uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji Monica Kassy (GS) (wa kwanza kushoto) wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu akiwa amefanikiwa kufunga goli wakati wa mechi kati ya timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Ikulu Rukia Kibayasa akimiliki mpira wakati wa mchezo dhidi ya Ikulu na Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi katika mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro.
Baadhi ya mashuhuda wa mchezo wa mpira wa pete kati ya Ikulu na Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Baadhi ya mashuhuda wa mchezo wa mpira wa pete kati ya Ikulu na Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
06/10/2014
Katibu wa Klabu ya
Ikulu Ramadhani Bendera ameipongeza klabu yake kwa kufanya vizuri katika
mashindano ya Shirikisho la Michezo ya watumishi wa Wizara na Idara za Serikali
(SHIMIWI) yanayoendelea mjini morogoro.
Bendera alitoa pongezi
hizo kwa klabu yake kufuatia ushindi waliopata katika michezo mbalimbali iliyochezwa
leo katika uwanja wa Jamhuri.
Timu za Ikulu zilizofanikwa
kuingia hatua ya robo fainali za mashindano hayo ni timu ya mchezo wa mpira wa
pete, mchezo wa kuvuta kamba wanaume na ya wanawake.
Katika mchezo wa mpira
wa pete, timu ya Ikulu imewabwaga timu ya Ulinzi kwa magoli 52-10 na hivyo
kuingia hatua ya robo fanali na kusubiria timu zitakazofuzu hatua hiyo.
Kwa upande wa mchezo wa
kuvuta kamba, timu ya Ikulu wanaume imeibuka washindi kwa kuwavuta timu ya
Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi 2-0 wakati timu ya wanawake ya Ikulu nao wameivuta
timu ya Wizara Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwa mizunguko yote miwili ambapo
hadi mwisho wa mchezo Ikulu wameshinda 2- Mifugo 0.
Aidha Bendera amesema
kuwa maandalizi mazuri ya klabu yake na wachezaji kujituma ndio msingi wa
ushindi wao wa leo kaatika michezo hiyo.
Mashindano ya SHIMIWI
nchini lengo lake kuwajengea watumishi afya bora na kujenga umoja wa kitaifa
kupitia Wizara na mikoa mbalimbali ambapo michezo inawakujenga ari ya ushindani
ndani ya watumishi wa umma na hatimaye kuleta ufanisi na tija kwa taifa wakati wakitekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
No comments:
Post a Comment