TANGAZO


Monday, October 6, 2014

Msanii Ali Kiba atembelea Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha Azania Flour Mills Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam

Na Kassim Mbarouk
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba ametembelea Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha Azania Flour, kinachomilikiwa na Kampuni ya Mikoani Traders, kilichopo Barabara ya Nyerere, Dar es Salaam.


 Nyota huyo, akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho, juzi jijini Dar es Salaam, alikipongeza kutokana na  uzalishaji wa bidhaa zilizo bora, zilizo katika ushindani wa Kimataifa, huduma bora sanjari na kutoa ajira kwa vijana Wakitanzania walio na elimu tofauti.
"Naamini kama si kiwanda hiki basi vijana wenzangu ambao wapo hapa wangekuwa katika maisha magumu mitaani na pengine hivi sasa wangelikuwa wakijishughulisha na kazi za haramu,"alisema.

"Wengine kutokana na ukosefu wa ajira wangekuwa katika matumizi ya dawa za kulevya na kujiweka katika mazingira hatarishi ambayo yangewasababisha kuishia katika vyombo vya dola," alisema.
Kwa upande wa uzalishaji wa bidhaa za kiwanda hicho, alikipongeza sana kwa kuliletea sifa taifa pamoja na kujali afya za walaji wa bidhaa hizo wa ndani na nje ya Tanzania.
"Ubora wa bidhaa zenu zenye viwango vya Kimataifa, sio sifa kwa kwenu nyinyi tu bali ni sifa ya Taifa zima na Tanzania pamoja na watu wake wote," alisema. 
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hizo, Ahmed Fuad, alisema anashukuru kwa ujio wa msanii huyo maarufu nchini na kuahidi kuwa atakuwa naye bega kwa bega katika shughuli zake za muziki ili kufikia mafanikio bora anayoyatarajia.
Aidha, alimpongeza kwa hatua kubwa aliyoifikia kimuziki na kumtaka kutotosheka na hatu hiyo, bali azidishe bidii kwani bidii ndio itakayomletea mafanikio zaidi.
Msanii Ali Kiba (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni za Mikoani Traders, Ahmed Fuad, wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusaga nafaka cha Azania, Barabara ya Nyerere juzi.
Msanii Ali Kiba na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni za Mikoani Traders, Ahmed Fuad, wakipozi kwa picha ndani ya moja ya Ofisi za Kiwanda hicho cha Kusaga Nafaka cha Azania, Barabara ya Nyerere.
Msanii Ali Kiba na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni za Mikoani Traders, Ahmed Fuad, wakiwa katika pozi.  


Msanii Ali Kiba (kulia), akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni za Mikoani Traders, Ahmed Fuad, wakati alipotembelea Kiwanda cha Kusaga nafaka cha Azania, Barabara ya Nyerere juzi.


No comments:

Post a Comment