TANGAZO


Monday, October 20, 2014

Shilingi milini 25 hutumika kufanya usafi Mbuga ya Mikumi, Morogoro

Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Mikumi Dattomax Sellanyika akiongoza zoezi la kufanya usafi katika Barabara Kuu ya Iringa Dar katika eneo la Hifadhi ya Mikumi pamoja na viongozi wa Mtandao wa habari za Kijamii Tanzania (MHAKITA)
Mratibu w Mtandao wa Hbari za Kijamii Tanzania, Ramadhani Libenanga na Ofisa Habari wa Mtandao huo, Latifa Ganzel wakifanya usafi katika eneo la Mbuga ya Mikumi pamoja na uongozi wa TANAPA.
Mratibu w Mtandao wa Hbari za Kijamii Tanzania, Ramadhani Libenanga na Ofisa Habari wa Mtandao huo,Latifa Ganzel wakifanya usafi katika eneo la Mbuga ya Mikumi pamoja na uongozi wa TANAPA.  (Picha zote na Peter Kimath)

Na Peter Kimath
Morogoro
KIASI cha sh milioni 25 hutumika kila mwaka katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kwaajili ya shughuli za usafi wa mazingira  na kuhudumia wanyama wanaogongwa katika barabara kuu iendayo Iringa na Morogoro.
Kaimu mkuu wa hifadhi ya Mikumi Dattomax Sellanyika , ameyasema hayo leo, wakati akizungumza na waandishi  habari waliotembelea katika hifadhi hiyo na kupata fursa ya kufanya usafi wa mazingira   kwa lengo la kupinga masuala ya ujangili kupitia mtandao wa habari za kijamii Tanzania MHAKITA.

Alisema kati ya fedha hizo milioni  12.5 hutumika kwaajili ya uokotaji wa takataka zinazotupwa na wasafiri wanaotumia barabara hiyo kwa kutotambua madhara ya taka hizo kwa wanyama waishio mbungani hapo.
Sellanyika alisema katika maeneo yaliowekwa  matuta  ili magari yaweze kupunguza mwendo kutokana na kuwa ni vivuko vya wanyama  pamegeuzwa ndio sehemu ya kutupa takataka kwa wasafiri hao.
Alisema utupaji wa takataka katika hifadhi hiyo una madhara makubwa kwa wanyama kwani baadhi ya takataka husababisha wanyama   kupoteza maisha wakizila.
Aliongeza kuwa  kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva kwenda mwendo kasi katika hifadhi, hiyo kinyume na sheria na kwamba kusababisha kuwagonga wanyama hasa nyakati za usiku wakati wanyama wanvuka barabara kuelekea upande wa pili wa mbuga.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya ikologia wa hifadhi hiyo Crispin mwinuka alisema  idadi ya wanyama wanaogongwa katika hifadhi hiyo wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika kipindi cha miaka 2009 hadi 2013 jumla ya wanyama 604 waligongwa katika barabara hiyo na kupoteza maisha.

Alisema mwaka 2012 wanyama waliogongwa walikuwa 111  huku mwaka 2014  walikuwa 132,katika kipindi hicho hicho jumla ya kilogramu 21,907.80 zilitupwa katika hifadhi hiyo na kusababisha hifadhi hiyo kuingia hasara kubwa katika kuokota taka hizo.

 Hata hivyo aliwataka  wasafiri wanaotumia barabara hiyo kujenga  tabia ya kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka katika vyombo vya usafiri ili kuepusha tatizo hilo na kuweza kuthibiti kabisa tatizo la uchafuzi wa mazingira kwani ni jambo ambalo linawekana kwa kila mwananchi

No comments:

Post a Comment