Katibu Mkuu wa Wizaraya Habari.Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akisalimia wananchi jana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana yanayofanyika katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.
Baadhi ya wadau wa wiki ya Vijana wakifuatilia Burudani kutoka kwa Kikundi cha JKT hakipo pichani jana mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya Vijana ambayo kitaifa inafanyika mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akielezea jambo alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na mwisho kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akielezea jambo alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana.Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga na mwisho kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Fatma Mwassa akiweka
saini katika kitabu cha wageni katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) jana mkoa Tabora mara baada ya kuzindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya
Vijana.
Baadhi ya wananchi wakipata
huduma ya upimaji wa afya zao katika banda la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
jana mkoani Tabora ambapo maadhimisho ya wiki ya vijana yanaenedele. (Picha zote na Frank Shija, WHVUM)
Na
Jonas Kamaleki - MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka
mkakati kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kutenga fedha
katika halmashauri mbali mbali nchini kwa lengo la kusaidia miradi ya vijana.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bibi
Fatma Mwassa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Wiki ya Vijana mjini Tabora leo
(jana). Bibi Fatuma amesema kuwa Mkoa wa Tabora umetenga jumla ya shilingi 1.8
kwa ajili ya kusaidia miradi ya vijana.
“Serikali inatambua changamoto zinazo wakabili
vijana ikiwemo ukosefu wa ajira ata hivyo tumekuwa tukijitahidi kukabiliana
nazo ikiwemo kwa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia vijana ambapo hapa mkoani
kwetu jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetengwa katiak halmashauri zote.”
Alisema Bibi. Fatma.
Aidha Bibi Fatma aliongeza kuwa Serikali ipo tayari
kusaidia Vijana katika kuendeleza shughuli zao na kuwataka kuwa wabunifu na
wenye dhamira ya kweli katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka vijana wasitumiwe tu na watu
wasioitakia mema nchi bali wajitambue ili waweze kufanya shughuli za uzalishaji
mali na kuacha tabia ya kukaa vijiweni. Pia amewaasa vijana kutojihusisha na
mada ya kulevya.
“Msitumike katika kubeba madawa hayo matumboni mwenu
au kuyauza reja reja,kataeni kutumikishwa,” alisisitiza Bibi Fatma Mwassa.
Amewataka vijana watumie fursa zilizopo ili waweze
kujiendeleza badala ya kulalamika. Amewaasa watumie ujana wao vizuri kama alivyoutumia
Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere ambaye tunaadhimisha miaka 15 ya
kifo chake. Alisema Mwalimu aliutumia ujana wake vizuri katika shughuli za
kisiasa na kujipatia heshima kubwa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga amesema kuwa Wiki ya Vijana
imekuwa jukwaa muhimu kwa Vijana wengi hapa nchini kwani upata fursa ya
kukutana na kujifunza kupitia maonyesho yanayoambatanana maadhimisho hayo.
Bibi. Sihaba aliongeza kuwa kumekuwapo na matokeo
chanya yanayotokana na maadhimisho hayo ambapo baadhi ya vijana wenye dhamira
wemepata kuwa wajasiriamali kupitia wa kubwa na wakati kupitia maadhimisho
hayo.
Wiki ya Vijana inaadhimishwa ikiwa inatimizwa umri
wa miaka 15 tokea ilipoanzishwa mnamo mwaka 2000 Mkoani Kilimanjaro. Katika
Wiki hii Vijana mbalimbali ujumuika pamoja katika maadhimisho hayo ambayo kwa
mwaka huu yanafanyoika mkoani Tabora na yatafikia kilele chake tarehe 14 Oktoba
ambayo ni siku ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na kilele cha mbio za Mwenge.
No comments:
Post a Comment