TANGAZO


Friday, October 10, 2014

Michuano ya Shimiwi: Timu za Utumishi na Ikulu zilivyopambana

Wachezaji wa Ofisi ya Rais,Utumishi na Ofisi ya Rais,Ikulu wakiruka juu kugombea mpira wakati wa mchezo wa nusu fainali wa mashindano ya SHIMIWI uliozikutanisha timu hizo katika kiwanja cha Jamhuri ,Morogoro. Utumishi imeingia fainali kwa kuifunga Ikulu magori 42 dhidi ya 41. (Picha na James Katubuka)
Baadhi ya washabiki wa mpira wa pete wakishuhudia mechi ya nusu fainali ya mashindano ya SHIMIWI kati ya Utumishi na Ikulu iliyochezwa   katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro. Utumishi imeingia fainali kwa kuifunga Ikulu magori 42 dhidi ya 41.
Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya  Utumishi Fatuma Machenga (GS) akifunga moja ya magori wakati wa mechi na nusu fainali ya mashindano ya SHIMIWI iliyozikutanisha timu yake na Ikulu katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.Utumishi imeingia fainali kwa kuifunga Ikulu magori 42 dhidi ya 41. 
Raha ya michezo ni ushindi, ndivyo wanavyoonekana  washabiki wa timu ya Utumishi wakiimba na kucheza mara baada ya  kumalizika kwa mechi ya nusu fainali ya mashindano ya SHIMIWI iliyozikutanisha timu hizo katika kiwanja cha Jamhuri, Morogoro.Utumishi imeingia fainali kwa kuifunga Ikulu magori 42 dhidi ya 41.

No comments:

Post a Comment