TANGAZO


Friday, October 24, 2014

Profesa Tibaijuka aongoa maadhimisho ya miaka 69 ya Umoja wa Mataifa (UN)

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka,ambaye alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akihutubia Dar es Salaam leo, katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 69 tangu kuundwa kwake. Maadhimisho hayo yamefanyika Viwanja vya Karimjee. 
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez, akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Tanzania na Mratibu Mkazi wa UNDP Tanzania, Alvero Rodriquez (kushoto) akiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, wakifuatilia matukio mbalimbali ya hafla hiyo.
Gwaride maalumu la maadhimisho hao.
Waziri Tibaijuka akihojiwa na wanahabri kuhusu maadhimisho hayo.
Wawakilishi wa mashirika ya kimataifa wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakisubiri kuondoka baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Gwaride maalumu la watoto la bendera likitoa heshima kwa mgeni rasmi.
Gwaride maalumu la vijana likitoa heshima kwa mgeni rasmi.
Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakichukua tukio hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za maadhimisho hayo.
Wanafunzi wa Shule ya Viziwi ya Buguruni wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Vijana wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo. 


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amehimiza nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za Mabadiliko ya Tabia Nchi miongoni mwao.
Tibaijuka alitoa wito huo leo, katika sherehe za kuazimisha miaka 69 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika katika viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Waziri Tibaijuka, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maazimisho hayo alibainisha kuwa mabadiliko ya Tabia Nchi yameendelea kuwa tishio kubwa kwa binadamu katika siku za leo duniani kote.
Kutokana na hali hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliitisha mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Septemba 23, mwaka huu ambapo watu, nchi, mabara na wafanyabiashara walitoa tamko la kuungana pamoja kwa kila mmoja kuinusuru dunia.
Prof. Tibaijuka alisema kuwa akiwakilisha bara la Afrika, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete aliwasilisha mpango unaoonyesha juhudi za pamoja zinazofanywa na bara hilo kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Katika mkutano huo, Tanzania imeahidi kuimarisha juhudi zake katika kutunza misitu na matumizi ya nishati kama upepo, sola na gesi asilia,” Waziri Tibaijuka alisema.

Hivyo Prof. Tibaijuka alihimisa nchi wahisani kutimiza ahadi zao kwa wakati hususani kutoa fedha kiasi cha dola za Kimarekani billion 100 kila mwaka hadi 2020 zitakazosaidia katika juhudi za kupambana na changamotio hizo.
Waziri aliwaambia wageni waalikwa katika sherehe hizo pia kuwa Tanzania inaendelea kutekeleza malengo ya changamoto za mileniamu na kuhakikisha kuwa nchi inaendelea kuimarisha amani, utawala wa sheria na kudimisha haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment