Waziri Mwinyi (wa pili kulia) akikaribishwa na Waziri William Lukuvi.
Akisaini kitabu cha wageni katika maombolezo hayo
Mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali Robert Mboma akisaini kitabu cha maombolezo.
Maafisa wakuu wa jeshi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu.
Mwinyi na Lukuvi wakielekea kuuaga mwili wa marehemu.
Mboma akitoa heshima zake za mwisho.
Ndugu na watoto wa marehemu wakiuaga mwili wa marehemu Kimario.
Mwili ukiwa katika gari maalumu.
Picha ya marehemu enzi za uhai wake.
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi aliongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu mstaafu Meja Jenerali Muhidin Kimario aliyefariki Oktoba 6 mwaka huu nchini India akipata matibabu.
Hafla hiyo imefanyika leo katika viwanja vya kambi ya Jeshi la Wananchi ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
Marehemu aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini pia. Baada ya kuagwa kwa heshima za kijeshi mwili ulipelekwa katika Msikiti wa Al-Mamur ulioko Upanga, jijini Dar e Salaam kwa ajili ya swala ambapo utasafirishwa kwenda kwao moshi kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
No comments:
Post a Comment