TANGAZO


Friday, October 10, 2014

Ufunguzi wa maadhimisho Siku ya Posta Duniani Oktoba 9, 2014


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Mkoma, akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na 
Teknolojia, Profesa Patrick Makungu akihutubia katika uzinduzi huo. Picha habari na mtandao wa www.habari za jamii.com.simu namba 0712-727062)
Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Lucy Mshomi wa Shule ya Wasichana ya Kifungiro kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mwalimu Josephine Mashare wa Shule ya Wasichana ya ST' Marys ya Mazinde Juu kutokana na mchango mkubwa kwa wanafunzi wao. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanafunzi mshindi wa kwanza kitaifa wa kuandika barua, Glory Mduma kutoka Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga. Kulia  ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi Mshindi wa tatu wa shindano hilo, Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya  ST, Marys Mazinde Juu. Kulia  ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta, Deus Mndeme.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu (kushoto), akimkabidhi zawadi mwanafunzi mshindi wa pili kitaifa wa kuandika barua , Ndehovye Nyindo  wa Shule ya Wasichana ya Lufungiro iliyopo mkoani humo. 
 Wanafunzi ambao ni washindi wa shindano la kuandika barua wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi zao walizokabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,  Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa katika hafla ya ufunguzi wa maadhimisho ya  siku ya Posta Duniani 2014 yaliyofanyika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni mshindi wa kwanza kitaifa wa shindano hilo, Glory Mduma kutoka Shule ya Sekondari ya ST, Marys Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa pili, Ndehovye Nyindo  wa Shule ya Lufingiro mkoani humo, na Mshindi wa tatu, Khadija Rashid wa Shule ya Sekondari ya  ST, Marys Mazinde Juu.
  Wanafunzi, Wazazi na wageni waalikwa wakiwa 
kwenye hafla hiyo.


Picha habari na mtandao wa www. habari za jamii.com.simu namba 0712-727062)

 Dotto Mwaibale

WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St Mary's ya Mazinde Juu iliyopo mkoani Tanga wameibuka vinara wa shindano la uandishi wa barua lililoshirikisha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini katika kuadhimisha siku ya posta duniani.
Shindano hilo la uandishi wa barua  limeratibiwa na Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na umoja wa posta duniani.
Akizungumza  Dar es saalam leo katika hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya posta duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Posta nchini,  Deus Mdeme  alitoa pongezi kwa washindi hao na walimu wao kwa kufanikiwa kuibuka videdea ambapo mshindi wa kwanza ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya barua ya kimataifa yatakayofanyika baadaye mwaka huu nchini Uswisi.

"Madhumuni ya shindano hili ni kuwajengea uwezo vijana ambao hawajazidi miaka 15'' alisema Mdeme.
 Katika Shindano hilo la uandishi wa barua jumla ya washindi kumi walipatikana, huku St Mary Mazinde juu wakiibuka videdea kwa kutoa washindi wawili huku mshindi wa pili akitoka Shule ya Sekondari ya
Lufingilo mkoani humo ambapo walikabidhiwa vyeti na zawadi mbalimbali.
Aidha katika kuadhimisha siku hiyo ya posta duniani, yenye kauli mbiu isemayo posta inachukua nafasi yake katika mageuzi ya sekta ya mawasiliano imeadhimishwa kwa kuelezea malengo na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Posta Tanzania.
Wakati huo huo Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Patrick Makungu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa, alielezea mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikabili Sekta ya Posta Tanzania katika kufanikisha malengo yake.

Vilevile alitumia nafasi hiyo kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika shindano hilo linaloandaliwa na umoja wa posta duniani na kuwataka wadau wa posta nchini kushirikiana na shirika hilo ili likue na kutoa huduma kwa jamii baada ya kubadilisha ufumo wa utoaji huduza zake kwa kutumia zaida Tehama..

No comments:

Post a Comment