TANGAZO


Wednesday, October 15, 2014

Mawaziri 7 wajiuzulu Nigeria

Rais Goodluck Jonathan
Mawaziri saba wa serikali nchini Nigeria wamejiuzulu nyadhifa zao katika serikali ya Rais Goodluck Jonathan.
Hatua ya mawaziri hao imekuja kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Februari mwaka ujao.
Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu hatua ya kujuzulu kwa mawaziri hao ingawa kuna dalili kuwa huenda wakajiuzulu ili kujitafutia nafasi kama magavana katika uchaguzi ujao.
Rais Goodluck Jonathan alitoa tangazo hilo katika mkutano wa baraza la mawaziri mjini Abuja.
Wale waliojiuzulu ni mawaziri wa mawasiliano, afya na wenzao wa elimu , ulinzi na wengineo.
Kujiuzulu kwao kutoka katika baraza la mawaziri, kulitarajiwa ingawa hawakutoa sababu za kuchukua hatua hiyo ila kuna taarifa kuwa huenda wanajiandaa kuwania nyadhifa za ugavana.
Wiki jana Rais Jonathan, alisema kuwa waziri yeyote aliye na hamu ya kunia nafasi yoyote yua kisiasa anapaswa kujizulu.
Magavana wa majimbo nchini Nigeria, wanaonekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa sababu ya pesa walizonazo au wanazopokea kutoka kwa serikali.
Baadhi ya wanigeria, wanaamini kuwa hii ndio moja ya sababu ya wanasiasa kufanya kila wawezalo ikiwemo kuiba kura ili kupata wadhifa wa gavana.
Wadadisi wanasema kuwa wanasiasa hutumia nyadhifa hizo hujinufaisha kifedha pamoja na washirika wao.

No comments:

Post a Comment