TANGAZO


Wednesday, October 15, 2014

Ulemavu sio hoja kwa shabiki Somalia

Ahmed Hassan Osman ni shabiki wa Chelsea
Ahmed Hassan Osman, ana umri wa miaka 20. Ni mlemavu wa macho na anaishi mjini Mogadishu. Alipoteza uwezo wake wa kuona akiwa na umri wa miaka saba.
Osman ni shabiki wa soka mchezo ambao wengi hawaushabikii sana. Anapenda ligi ya Uingereza na yeye hutembea hadi katika viwanja vya mipira ambako mechi hufanyika. Pia huenda katika kumbi mbali mbali ambako michuano ya ligi ya Uingereza huionyeshwa kupitia kwa televisheini.
Mwandishi wa BBC Ibrahim Mohamed Aden ambaye yuko mjini Mogadishu alikutana na Osman na kumuuliza kuhusu mapenzi yako ya soka.
Ahmed: Nilipenda sana soka kabla ya kupoteza uwezo wangu wa kuona , nilikuwa nikicheza sana soka na nilipopoteza uwezo wangu wa kuona niliendelea kujaribu kucheza soka.
Ibrahim: Sasa hivi uko katika uwanja wa michezo je unafuatlia vipi mchezo?
Ahmed: Kwanza hisia zangu nyinginezo ziko hai hasa mchezo unapokuwa unaendelea, nina maskio kwa hivyo ninaweza kusikia watu wakishangilia. Nadhani mimi hufuatilia mchezo sawa tu na mashabiki wengine wanavyokuwa.
Ibrahim: Na unajua vipi matokeo ya mchezo?
Ahmed: Mimi huhesabu idadi ya mabao, ninaposikia watu wakishangilia na kuongea, hivyo ndivyo mimi huhesabu matokeo.
Ibrahim: Na pia wewe ni shabiki sugu wa ligi ya uingereza au?
Ahmed: Ndio ndio, mimi napenda sana ligi ya Italia kwa sababu ndio iliyokuwa inashabikiwa sana nchini humu. Baadaye watu wakaanza kutazama ligi ya Uingereza. Kwa sasa msimu huu ni mgumu sana. Timu zote ni nzuri na zinaonekana kutoshana nguvu.
Ibrahim: Wewe ni shabiki wa timu gani?
Ahmed: Napenda sana Chelsea. Tangu Mrusi Abramovij,kuinunua , imekuwa ikifanya vyema sana. Aliwekeza sana kwa timu hiyo na ninapenda wachezaji wake. Na najua kama wachezaji wengi wa Chealsea wana asili ya kiafrika. Kwa hivyo kwa sababu tuna wachezaji wengi wazuri, tunaongoza ligi kwa sasa naamini kama tutamaliza washindi.
Ibrahim: Kwa sasa wewe ni mtu tofauti sana, nimeona watu wengi vipofu ambao walipoteza matumaini yao katika maisha mjini Mogadishu.
Ahmed: Mimi huwaambia kila binadamu ana unyonge wake. Sio walemavu peke yao, hata wale ambao hawana ulemavu wowote , wote wana unyonge fulani. Na kwangu mimi sioni ulemavu wangu kama ni changamoto maishani mwangu.

No comments:

Post a Comment