TANGAZO


Wednesday, October 15, 2014

Tisho la Al-Shabaab kushambulia Ethiopia

Wapiganaji wa Al Shabaab
Marekani imeonya kuwa wapiganaji wa Kiislamu wa Al shabaab wanapanga kufanya mashambulio katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.
Taarifa iliyotolewa na balozi ya Marekani mjini Addis Abbaba imeonya kuwa wanangambo hao wa Al Shabaab wamepanga kushambulia wilaya ya Bole ambayo ofisi za balozi nyingi za mataifa ya kigeni zipo pamoja na uwanja wa kimataifa wa ndege.
Wanajeshi wa Ethiopia wanaendeleza harakati za kupambana na kundi hilo la Al Shabaab nchini Somalia kama sehemu ya kikosi cha muungano wa Afrika.
Kundi la Al Shabaab sasa limetishia kuwa kundi ambalo lina wapiganaji wake katika nchi nyingi hasa kufuatia mashambulo ya hivi karibuni nchini Kenya na Djibouti.
Ripoti ya hivi karibuni iliyochapishwa na wachunguzi wa umoja wa mataifa lilisema kuwa mashambulo yaliyopangwa na kundi hilo nchini Ethiopia yalitibuliwa.

No comments:

Post a Comment