Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu
utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji na
Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Richard Sezibera,
wakati wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na
Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika majadiliano kuhusu
utengamano wa Afrika na Fursa za biashara na Uwekezaji, na
baadhi ya viongozi, Katibu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Balozi Richard Sezibera (katika) na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Ghana, Hanna Tetteh, wakati
wakihojiwa na Mwandishi wa habari wa Kimataifa na Mkurugenzi
wa Kampuni ya ‘Eddo Media’, Mark Eddo (kushoto).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na
|
Mohammed Gharib Bilal (wa nne kutoka kulia) akijumuika na
baadhi ya viongozi wakati alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.
Baadhi ya Washiriki wa kongamano hilo kutoka Tanzania,
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
Nehemiah Mchechu (wa tatu kutoka kulia), akijadiliana jambo na
Prof. Ahmada Khatib kutoka Tume ya Utalii Zanzibar wakati
walipohudhuria mkutano huo, uliofanyika katika Hoteli ya Atlantis
nchini Dubai. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal (wapili kulia) akisalimiana na baadhi ya
wageni pamoja na viongozi, alipohudhuria Mkutano wa GBF, uliofanyika kwenye Hoteli ya Atlantis jijini Dubai.
Na Mwandishi wetu, Dubai
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Oktoba Mosi, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika kongamano la pili la Kimataifa la Biashara kwa nchi za Afrika lililofanyika katika jiji la Dubai, Farme za Kiarabu.
Kongamano hili limehudhuriwa na washiriki wapatao 800 kutoka nchi mbalimbali duniani na limelenga katika kukuza uwekezaji katika nchi za Farme za Kiarabu na kufungua fursa za kibiashara barani Afrika. Kongamano la kwanza la namna hii lilifanyika pia jijini hapa mwaka jana na kushirikisha washiriki wapatao 3000 kutoka nchi mbalimbali duniani.
Baadhi ya Viongozi wa Afrika waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais John Dramani Mahama wa Ghana na Rais Mulatu Teshone Watu wa Ethiopia.
Viongozi hawa kwa nyakati tofauti walizungumzia umuhimu wa utengamano barani Afrika na wakaeleza kuwa hiyo ndiyo fimbo pekee ya kukuza uwekezaji wenye tija Afrika.
Pia walizungumzia mabadiliko makubwa ya Afrika huku wakiwakumbusha wawekezaji na wafanyabiashara waliohudhuria kongamano hilo kuwa Afrika ya sasa siyo bara la giza na kwamba ni bara linalokuwa kimaendeleo kwa kasi huku likiwa na fursa ya kukuza maendeleo yake kwa haraka.
No comments:
Post a Comment