*Yaiondoa Tamisemi kwa mikwaju ya penalti 4-3
Wachezaji wa timu ya
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiomba dua kabla ya mchezo wa
hatua ya mtoano katika mashindano ya SHIMIWI leo uwanja wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).Mashabiki wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakishangilia ushindi wa timu yao baada ya kuifunga timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) magoli 4-3 kwa njia ya mikwaju ya penati baada mchezo huo kuisha kwa suluhu ya kutokufungana.
Picha ya pamoja yaViongozi,
wachezaji na mashabiki wa timu ya Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifurahia ushindi wao dhidi ya timu
ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika
mashindano ya SHIMIWI yanayoendelea mjini Morogoro. (Picha zote na Eleuteri
Mangi -MAELEZO)
(Na Eleuteri Mangi –
MAELEZO)
04/10/2014
Timu ya mpira wa miguu
ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeibuka kidedea kwa kuifunga
timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mikwaju ya penati 4 – 3.
Ushindi huo wa timu ya Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo umetokana na kazi nzuri aliyoifanya mlinda
mlango wao Ramadhani Mtenga ya kupangua penati ya kwanza kuelekezwa langoni
mwake.
Ujasiri huo wa mlinda
mlango ndio uliotoa hamasa kwa wachezaji na mashabiki wa Wizara ya Habari Vijana,
Utamaduni na Michezo ya kupata ushindi katika mchezo huo.
Wachezaji waliyoipatia
ushindi timu yao waliongozwa na Edward Boniphance aliyefunga penati ya kwanza, penati
ya tatu ilifungwa na Mbozi Katala, ya nne alifunga Ahmed Salimu na penati
iliyowahakikishia ushindi Habari ilifungwa na Carlos Mlinda ambaye pia ni
Nahodha wa timu hiyo huku James Mapepele akikosa kufunga penati ya pili.
Ushindi huo umeifanya
timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kuingia hatua ya timu
16 katika mashindano hayo ya SHIMIWI yanayotarajiwa kufikia kilele Oktoba 11
mwaka huu.
Kikosi kamili
kilichoibwaga timu ya TAMISEMI kiliongozwa na Nahodha Carlos Mlinga na Mlinda
mlango Ramadhani Mtenga.
Wachezaji wengine ni
Erick Mfugale, Noel Kambona, Hashimu Yusufu, Mbozi Katala, Milinde Mahona,
Maurus Ndenda, James Mapepele, Ahmedi Salimu na Edward Boniphance.
Wachezaji wa akiba
katika kikosi cha timu ya Habari walikuwa Idrisa Michael, Ayubu Abdallah,
Hussein Makame na Pasto Mwita.
Wakati benchi la ufundi
liliongozwa na mwalimu Tunge Shem, Daktari wa timu Biondo Ngome pamoja na
Mwenekiti wa timu ya Wizara hiyo Dkt. Magreth Mtaki.
Aidha, Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekuwa Wizara ya kwanza kupata ubingwa
katika mashindano ya SHIMIWI katika mchezo wa kurusha tufe ambapo mchezaji
Mohamedi Mkangara amekuwa mshindi wa kwanza kwa kurusha tufe kwa umbali wa mita
11.32 ambao hakuna mchezaji mwingine aliyefikia umbali huo katika mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment