TANGAZO


Saturday, October 4, 2014

Mahafali ya Tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi yafanyika viwanja vya Makao Makuu ya bodi hiyo, Dar es Salaam leo

Mkurugenzi wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Dk. Clemence Tesha (kushoto) akiwaapisha wahitimu wa shahada ya kwanza  ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi, kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam leo.
Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakionekana wenye furaha muda mfupi baada ya kutunukiwa vyeti, stashahada na shahada za ununuzi na ugavi kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam leo.
Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakila kiapo cha utii na uaminifu muda mfupi baada ya kutunukiwa vyeti, stashahada na shahada za ununuzi na ugavi kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Sr. Dk Hellen Bandiho, akizungumza na wahitimu mbalimbali wa vyeti, stashahada na shahada za ununuzi na ugavi kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam, katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dorothy Mwanyika, na Mkurugenzi wa Bodi hiyo, Dk Clemence Tesha.
Wahitimu wa Mahafali ya tano ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya tano yaliyofanyika kwenye viwanja vya bodi hiyo, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment