*Zatoka sare ya bao 1-1
*Stand wakamia mchezo
Wachama na Mashabiki wa Simba wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Stand United ya Shinyanga, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Timu hizo zilitoka sare kwa kufungana bao 1-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Emmanuel Okwi (katikati) wa Simba akiwa amezongwa na Idd Mobby (kulia) na Mussa Said wa Stand United, wakati wa mchezo huo.
Hamis Tambwe (kulia) wa Simba akimtoka Idd Mobby wa Stand United.
Hamis Tambwe wa Simba akikwatuliwa na Idd Mobby wa Stand United.
Hamis Tambwe wa Simba na Idd Mobby wa Stand United, wakiwa wameanguka chini.
Hamis Tambwe (kushoto) wa Simba akiwania mpira na Idd Mobby wa Stand United.
Emmanuel Okwi (kulia) wa Simba akikimbilia mpira pamoja na Swaleh Abdallah wa Stand United.
Emmanuel Okwi wa Simba akiwekwa chini na Swaleh Abdallah wa Stand United.
Emmanuel Okwi (mbele) wa Simba akiwahi kunyanyuka na kukimbia mpira huku akifuatwa na Swaleh Abdallah wa Stand United.
Emmanuel Okwi wa Simba akiwekwa tena chini baada ya kukatwa na Idd Mobby (aliyelala), wakati akikimbia mpira kuelekea langoni mwa Stand United.
Mohamed Hussein wa Simba, akiwania mpira na Salum Kamana wa Stand United.
Salum Kamana wa Stand United, akimtoka Mohamed Hussein wa Simba.
Elias maguri wa Simba, akiudhibiti mpira huku akifuatwa Salum Kamana (kushoto) wa Stand United.
Patashika kwenye lango la Stand United wachezaji wakiruka kuupiga mpira kichwa baada ya kuchongwa kona kwenye lango hilo.
Emmanuel Okwi (kulia) wa Simba akipambana na Idd Mobby (kushoto) na Swaleh Abdallah wote wa Stand United.
Emmanuel Okwi (kulia) wa Simba akiwania mpira na Idd Mobby wa Stand United.
No comments:
Post a Comment