Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya
Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John
Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa
na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa
wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa
mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera.
(Picha na Hassan silayo-maelezo)
Na
Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama
ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira
yake ya haki sawa kwa wote ili
kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na
rufaa kukaa Mahakamani kwa muda mrefu.
Hayo
yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary
Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Akizitaja
hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha bajeti ya
kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni 57 kwa mwaka
2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya Mahakama ya Rufani
vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka 2013/14.
Aidha,
Bi Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha kitengo cha Mahakama
Kuu Dar es Salaam kitakacho shughulikia masuala ya utatuzi wa mashauri kwa njia
ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati ya kanuni za Mahakama itakayosaidia
kutunga au kurekebisha kanuni ili kuhakikisha kuwa kanuni zinazotumika
Mahakamani si chanzo cha kuchelewa mashauri Mahakamami.
Naye,
Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka
Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama imeanza kuchukua
hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na maadili ya watumishi kwa
kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili.
Aidha,
Bw. Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji anatakiwa kuvitimiza
kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa Mahakamani kuwa ni Mh. Jaji wa
Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na
Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa Mahakama za mwanzo kesi 260.
Mahakama
Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe zinazopangwa ili
kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa Mahakamani.
No comments:
Post a Comment