Mkuu
wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania Bw. Comfort
Komba akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) Kuhusu mafanikio
yaliyofikiwa na Ofisi hiyo ikiwamo ujenzi wa majengo ya chuo cha ukutubi na
uhifadhi wa nyaraka kilichopo Bagamoyo na uzinduzi wa maktaba za wilaya za
Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu, wakati wa Mkutano
uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Bi. Georgina Misama. (Picha na Hassan Silayo, Maelezo)
Na
Hassan Silayo-MAELEZO
Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania imeanzisha masomo ya jioni ya diploma ya ukutubi katika
Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015.
Hatua
hiyo inatokana na kuongezeka kwa maombi ya wanafunzi wanaohitaji kuendelea na
masomo baada ya kuhitimu mafunzo ya cheti.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba
Tanzania Bw. Comfort Komba wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini
Dar es Salaam.
Comfort
alisema kuwa masomo hayo kwa awali yalikuwa yakitolewa katika kampasi ya
Bagamoyo lakini kutokana na kuongezeka kwa uhitaji wa masomo hayo ambapo mpaka
sasa kuna wanafunzi wapya 130.
“Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania imeamua kuanzisha masomo ya jioni ya diploma ya
ukutubi katika Kampasi ya Dar es Salaam katika mwaka wa masomo 2014/2015 na
utaratibu huu tunautekeleza kutokana na kuwepo kwa ongezeko la uhitaji wa
wanafunzi” Alisema Comfort.
Aidha
Comfort alisema kuwa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania kwa kushirikiana na
halmashauri za Wilaya na Mikoa imefanikiwa kuanzisha maktaba katika wilaya
mbalimbali ikiwemo Kibaha, Chunya, Ruangwa, Ngara, Rulenge, Masasi na Mbulu.
Akizungumzia
kuhusu uhufadhi wa machapisho ya kitaifa, Comfort alisema kuwa Ofisi hiyo imefanikiwa kuhifadhi
jumla ya vitabu 1,300,000 pamoja na majarida 950,000 tangu Bodi hiyo
ilipoanzishwa katika ngazi ya Mikoa, Wilaya hadi Tarafa.
Bodi
ya Huduma za Maktaba Tanzania ni Shirika la umma lililopo chini ya Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
No comments:
Post a Comment