TANGAZO


Wednesday, October 22, 2014

NHIF yaanzisha mpango wa kupeleka Madaktari Bingwa Mikoani

 Mkurugenzi wa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Raphael Mwamoto, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,  kuhusu mpango wao wa kupeleka Madaktari bingwa mikoani kutoa huduma mbalimbali za tiba. 
 Mwamoto akifafanua jambo katika mkutano huo, ambapo alisisitiza wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii na NHIF ili wakati wa mpango huo, wapate unafuu wa gharama za matibabu.
Mwamoto akieleza jinsi mpango huo, ulivyofanikiwa katika awamu ya kwanza iliyofanyika katika Mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma na Lindi ambapo walitumia zaidi sh. mil 180. (Picha zote na Kamanda Richard Mwaikenda)
 Mwamoto akielezea kuwa Madaktari bingwa hao, wanatokea Hospitali za Muhimbili, Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Bugando Mwanza. Alisema kwamba Madaktari hao, kuwa ni Mabingwa wa Magonjwa ya moyo, wanawake, watoto, upasuaji na wa dawa za usingizi. Kushoto ni Meneja Utafiti na Ubora wa NHIF, Dk. Mkwabi Fikirini.
 Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya NHIF, Dar es Salaam.
 Waandishi wa hahabari wakiwa katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment