Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar Dkt. Abdalla
Ismail Kanduru akitoa tamko la kuwatunuku stashahada wahitimu wa Chuo
hicho katika Mahafali ya 21 yalifanyika Mbweni.
Wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Afya Zanzibar wakila kiapo cha utiifu
mbele ya mgeni rasmi Balozi Seif Ali Iddi katika mahafali ya 21
yaliyofanyika chuoni Mbweni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na
wahitimu wa Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Zanzibar katika Mahafali
ya 21 yaliyofanyika Chuoni Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Wa
kwanza kulia ni Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Dkt. Abdalla Ismail Kanduru.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtunuku
zawadi Mhitimu Leila Ali kwa kuwa miongoni mwa wanafunzi waliofanya
vizuri zaidi katika mahafali ya Chuo cha Taaluma za Afya Mbweni
Zanzibar.
Wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo hicho wakimsikiliza mgeni rasmi
(hayupo pichani) baada ya kuwatunuku stashahada katika mahafali ya 21.
Wageni waalikwa walioshiriki mahafali ya 21 ya Chuo cha Taaluma za Afya
Zanzibar wakifuatilia maadhimisho hayo yaliyofanyika Chuoni, Mbweni. (Picha zote kwa hisani ya Otman Maulid wa ZanziNews)
No comments:
Post a Comment