Mkufunzi wa timu ya Manchester Louis van Gaal amesisitiza kuwa hakuchukuwa jukumu kubwa la kumfanya Jose Mourinho kuwa miongoni mwa wakufunzi waliofaulu duniani.
Mkufunzi huyo wa Chelsea aliyefanya kazi chini ya Van Gaal katika kilabu ya Barcelona amekuwa akimsifu Kocha Van Gaal kwa mafanikio yake pamoja na Bobby Robson.
''Amekuwa akizungumza kunihusu na namshukuru kwa hilo lakini amekuwa akijifanyia mwenyewe'' alisema Van Gaal.
Wawili hao watakutana katika uwanja wa Old Trafford siku ya jumapili wakati ambapo Manchester United itakutana na Chelsea.
Kwa mara ya kwanza walikutana miaka 17 iliopita wakati Van Gaal alipomkabidhi Mourinho kazi katika kamati ya kufunzi katika uwanja wa Barcelona.
No comments:
Post a Comment