TANGAZO


Tuesday, October 21, 2014

Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits yasisitiza utii wa Sheria bila shuruti

Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, James Rugemalira  (kushoto), akigongeana glasi na wakili maarufu wa kampuni hiyo, Michael Ngalo.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Benadicta Rugemalira (Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kushoto ni Mke wa wakili, Camilo Schutte kutoka Uholanzi, Lize Schutte, Padri wa Kanisa Katoriki Parokia ya Himo, Fabian Nderumaki, Wakili Schutte na wakili kutoka Marekani, Chris Provenzano.
Katibu Mtendaji wa Kata ya Marangu Magharibi,  Rose Lyimo (anayeangalia kamera), akifurahia kinyaji bora cha windhoek na wageni wengine waalikwa.
Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo huku wakipata kinywaji bora cha Windhoek Draught.
Viongozi wa Kampuni ya Mabibo na mawakili kutoka Ulaya na Marekani wakipata maelezo juu ya soko la bia aina ya Windhoek kutoka kwa Meneja Mkuu wa Nymbani Hotels and Resort Mansuetha Michael (hayupo pichani). 
Wadau mbalimbali wakibadilishana mawazo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa kampuni ya Mabibo namna ya kuzingatia sheria bila shuruti.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo,  Benedicta Rugemalira akimwelekeza Meneja Mkuu wa Nyumbani Hotels and Resort Mansuetha Michael namna ya kuitambua bia za Windhoek halali zinazotakiwa kuweko kwenye soko la Tanzania zenye code namba ubavuni MB66.
Mrembo wa Hoteli ya AMEG Lodge Kilimanjaro,  Miriam Ismail akipeleka vinywaji vya Windhoek kwa wateja. 
Mzee Rugemalira akitoa maelezo mafupi juu ya ubora wa bia ya Windhoek. 
Mrembo wa Hoteli ya AMEG Lodge Kilimanjaro, Miriam Isumail (kushoto), akiwa na mrembo mwenzie, Modesta Dennis. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited yenye haki pekee ya kuagiza na kusambaza kinywaji aina ya Windhoek katika soko la Tanzania imetoa wito kwa wakazi wa mji wa Moshi na vitongoji vyake kuzingatia dhana ya utii wa sheria bila shuruti. Wito huo ulitolewa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa kampuni hiyo, James Rugemalira, jana usiku katika hoteli ya Kilimanjaro Mountain Resort iliyoko katika maeneo ya Marangu, Moshi mkoani  Kilimanjaro, alipokutana na wadau mbalimbali. 

“Naomba kuwakumbusha kuwa kuna amri ya Mahakama ambayo inazuia mtu yeyote kuingiza na kusambaza Windhoek katika soko hapa nchini bila kuomba na kupata kibali kutoka Mabibo. Amri hii ni halali na inapswa ifuatwe,”  alisisitiza Rugemalira. 

Akiwa ameambatana na mawakili wake kutoka nje ya nchi na hapa nchini, Rugemalira alisisitiza kuwa bia aina ya Windhoek inayopaswa kuuzwa katika soko la Tanzania lazima iwe na alama ya MB66 na kwamba inasabazwa na kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. “Hivi sasa tunatumia muda huu kutoa elimu na namna ya kuzingatia sheria bila shuruti. Lakini muda utafika na tutawashughulikia wale wote watakao kiuka amri hii,” alisema. 

Katika hafla hiyo, wageni mbalimbali walihudhuria, akiwemo Katibu Mtendaji wa Kata ya Marangu Magharibi, Rose Lyimo. 

Rugemalira aliwaomba wananchi kushirikiana na kampuni yake kwa kununua bia halali iliyolipiwa kodi ili kuweza kupanua soko ambalo litawezesha kampuni yake kuanza kuzalisha aina hiyo ya bia hapa nchini. Kwa sasa kampuni ya Mabibo inaagiza bia aina ya Windhoek kutoka Namibia. “Tunategemea kujenga kiwanda hapa nchini cha kuzalisha Windhoek. Maeneo ambayo tumeona yanafaa ni pamoja na hapa Moshi. Lakini pia tunaweza kufanya hivyo aidha Tanga au Kagera. Hivyo tushirikiane ili tujenge nchi yetu kwa pamoja na tuepuke kununua bidhaa za magendo,” alisisitiza. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment