Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha karatasi kwa kutumia Gesi
Asili iliyozalishwa na Mtambo huo. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
Tuesday, October 21, 2014
Chuo Kikuu Ardhi kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na taka ngumu
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa
habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na jitihada za
kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu ikiwemo ujengaji wa
miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu
au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na gesi asili ya kupikia,
wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibiolojia
zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste
treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika
na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa
ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa
kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi
zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa
Mshoro
Mkemia
Mkuu wa Kiwanda cha Mansoor Daya Chemicals Bw. Benedict Mtenga Akiwaeleza
waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi wanavyoendelea kunufaika na
teknolojia hiyo ya kibiolojia ikiwemo kutumika kusafisha maji taka
yanayozalishwa na kiwanda hicho na kuepusha uharibifu wa mazingira,wakati wa
ziara iliyofanywa katika kiwanda hicho ili kuona jinsi teknolojia inavyofanya
kazi.
Miundombinu
ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka
ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu
cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya
Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals
Miundombinu
ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka
ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu
cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya
Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals
Miundombinu
ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka
ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu
cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya
Binadamu cha Mansoor Daya Chemicals
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo na kutembelea maeneo
ilipojengwa miundombinu ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili taka ngumu au
maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza
Selele akiwaeleza waandishi wa habari jinsi mtambo wa kuzalisha gesi asili
inayotokana na mabaki ya chakula, taka za jikoni na mbogamboga, wakati wa ziara
iliyofanywa chuoni hapo kujionea jinsi teknolojia ya kubadili taka ngumu na
kuzalisha gesi asili ya kupikia inayofanya kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment