Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo wa mpira wa pete kati ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo na Polisi leo mjini Morogoro.
Na Eleuteri Mangi-
MAELEZO
28/09/2014
SHAMRASHAMRA za mashindano
ya Shirikisho la Michezo ya watumishi
Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) zimepamba moto kwa timu mbalimbali
kumenyana katika michezo mjini morogoro.
Wizara ya Habari,
Vijana Utamaduni na Michezo leo wameanza vema mashindano hayo kwa kuwapa
kichapo timu ya Polisi kwa mchezo wa mpira wa pete kwa kuwachapa magoli 45 kwa
01 dhidi ya wapinzani wao na kuibuka washindi katika mechi hiyo.
Ushindi huo umetiwa
hamasa ambapo wachezaji hao wanatambua kuwa Wizara hiyo ndio yenye dhamana ya
kusimamia michezo nchini.
Wakicheza kwa umahiri,
huku wakitambua kuwa wao ndio wanaopaswa kutoa mfano kwa timu nyingine
zinazoshriki mashindano hayo,wacheaji hao walizitumia idara zote katika mchezo
huo kikamilifu hivyo wailioibuka kidedea katika mchezo huo.
Akizungumzia ushindi
wao Nahodha wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Johari
Kachwamba amesema kuwa siri ya ushindi huo ni nidhamu na kuzingatia maelekezo
ya mwalimu na mazoezi wakati wote wa maandalizi ya mashindano hata wakati wa
mashindano yanayoendelea.
Kachwamba amesema kuwa
wanaendelea kujifua na hawabweteki na ushindi huo walioupata leo kwani
mashindano mashindano ndio yanaanza.
Aidha, timu ya kuvuta
kamba wanaume ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeshinda baada
ya timu ya RAS Tanga kutokutokea uwanjani hapo, hivyo kujihakikishia nafasi ya
kusonga mbele katika hatua inayofuata.
Mechi zilizochezwa leo
uwanja wa Jamhuri Morogoro ni pamoja na kuvuta kamba wanawake kwa wanaume, mpira
wa pete, na mpira wa miguu ambapo mwaka huu timu 54 zinashiriki mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment