Watumishi wa Serikali kutoka Wizara na Idara za Serikali wakiwa kwenye maandamano kabla ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
Watumishi wa Serikali kutoka Wizara na Idara za Serikali wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (hayupo pichani), wakati wa ufunguzi wa mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Morogoro leo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bw.Noeli Kazimoto akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kabla ya ufunguzi rasmi wa michezo ya SHIMIWI mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (kushoto) akisalimiana na wageni waalikwa na viongozi mbalimbali wa serikali alipowasili kwenye viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya SHIMIWI.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb) akifungua mashindano ya michezo ya SHIMIWI mjini Dodoma leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu zinazoshiriki michezo hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu zinazoshiriki michezo hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani, akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu zinazoshiriki michezo hiyo.
Na Happiness Shayo
WAAJIRI katika Wizara, Idara
Zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali wametakiwa kuhakikisha kuwa
wanaweka bajeti ya kutosha na utaratibu mzuri wa michezo kwa watumishi wao ili
kujenga ukakamavu, afya na pia kufahamiana.
Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh.Celina O. Kombani (Mb)
alisema hayo leo alipokuwa akifungua mashindano ya SHIMIWI mjini Morogoro.
“Pamoja
na changamoto za ufinyu wa bajeti na kuwa na kazi nyingi,waajiri wanatakiwa
wadumishe michezo sehemu za kazi”alisema Mh. Kombani.
Mh. Kombani
alifafanua kuwa pamoja na mambo mengine michezo inaepusha maradhi ya mara kwa
mara hasa yanayosababishwa na uzito uliokithiri.
Aidha, Mh. Kombani
aliwataka wanamichezo kuwa na mshikamano na kushirikiana katika kipindi chote
cha michezo.
Awali
akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
wa Morogoro Bw. Noeli Kazimoto aliwataka wanamichezo wanaoshiriki SHIMIWI
wazingatie maadili ya Utumishi wa Umma hata kama wako nje ya vituo vyao vya
kazi.
“Lazima
tuzingatie maadili na kudumisha nidhamu tunapoendelea na michezo hii kwa kuwa
sisi bado ni watumishi wa Umma”alisema Bw.Kazimoto.
Akimkaribisha
mgeni rasmi kufungua mashindano hayo, Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Danieli
Mwalusamba alitoa shukrani kwa uongozi wa mkoa wa Morogoro kwa kutoa
ushirikiano wa kutosha hadi kufanikisha mashindano hayo.
Wakati
huohuo, timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Timu
ya mpira wa miguu ya Mkoa wa Arusha zilitoka bila kufungana baada ya mechi za
ufunguzi kuanza huku timu ya netiboli ya Ikulu ikishinda kwa kete 62 dhidi ya
timu ya Mkoa wa Morogoro iliyoambulia kete 10.
Kwa
upande wa timu za kamba, timu ya wanaume ya Ikulu iliibuka mshindi kwa pointi 2
baada ya kuiburuza timu ya kamba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa huku timu ya kamba wa wanawake ya Wizara ya Uchukuzi ikiibuka kidedea
baada ya kuivuta timu ya kamba ya wanawake ya Mkoa wa Iringa na kushinda kwa
pointi 1.
Shirikisho la Michezo ya Wizara
na Idara za Serikali (SHIMIWI) huandaa
mashindano yanayowakutanisha watumishi wa Serikali kila mwaka lengo kuu ikiwa
ni kuendeleza tabia ya ushirikiano, upendo na undugu.
No comments:
Post a Comment