Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
28/09/2014
MWALIMU wa timu ya Ikulu inayoshiriki mashindano ya
Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) George Mbilinyi
amewapongeza wachezaji wa timu yake ya
mpira wa miguu, benchi lao la ufundi
na washabiki kwa kufanikisha ushindi wao
muhimu katika mashindano hayo.
Timu ya Ikulu
ilianza mchezo vizuri kipindi cha kwanza na cha pili na kuwapelekea hadi mwisho
wa mchezo kuwashinda Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mabao
2-0 katika mchezo uliochezwa leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini
Morogoro.
Mbilinyi amesema kuwa ushindi huo umetokana na ushirikiano kutoka
kwa wachezaji walioonesha kiwango
kikubwa katika mchezo huo wakiongozwa na kiwango cha kujituma uwanjani.
Mbilinyi amesema kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, wapinzano wao walikosea na wao wakatumia nafasi hiyo kupata ushindi huo mnono wa mechi ya kwanza.
Mbilinyi amesema kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa makosa, wapinzano wao walikosea na wao wakatumia nafasi hiyo kupata ushindi huo mnono wa mechi ya kwanza.
Naye Nahodhaa wa timu ya Ikulu Amos Ndege amesema
kuwa mchezo huo umewapa hamasa na nguvu ya kujiandaa na mchezo wao unaofuata
ili waendelee kufanya vizuri zaidi.
Aidha, Ndege amesema kuwa uwanja waliotumia
unachangamoto kubwa kwani unahitaji kuandaliwa vizuri kwa ajili ya mashindano
hayo muhimu kwa ajili ya kujenga afya bora za watumishi wa Serikali na
watumiaji wengine wa uwanja huo.
Kwa upande wake Mwalimu wa timu ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na MichezoTunge Shem amesema kuwa wanaendelea na maandalizi
ya mchezo unaofuata na anayafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa
kwanza ili waweze kuibuka kidedea katika mchezo unaofuata.
Vilevile Nahodha wa timu ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo Carlos Mlinda amesema kuwa wachezaji wa timu yake wote
wapo fiti kukabiliana kesho na timu ya RAS Simiyu.
No comments:
Post a Comment