Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo waki wa katika picha ya pamoja
kabla ya mtanange dhidi ya RAS Simiyu leo katika viwanja vya Chuo Kikuu cha
Sokoine cha Kilimo (SUA) mjini Morogoro.
1 Waamuzi wa mchezo mpira wa miguu kati ya
timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na RAS Simiyu
wakiongozwa na mwamuzi wa kati Ramadhani Omari (wa pili kulia) wote kutoka
kituo cha michezo ya vijana chini ya miaka 20 kijulikaanacho kama Twalipo cha
mjini Morogoro.
Wachezaji Johari Kachwamba (kulia) na
Hadija Omari Jaa (kushoto) wakiwa kwenye harakati za kuwania mpira wakati wa
mechi kati ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. (Picha
zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri
Mangi-MAELEZO
29/09/2014
Timu ya mpira wa miguu
ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imejiweka kwenye nafasi nzuri
ya kusonga mbele katika mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Watumishi wa Wizara
na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayoendelea mjini Morogoro.
Wakicheza kwa kuonana
timu hiyo ikiongozwa na Nahodha wao Carlos Mlinda walilisakama lango la
wapinzani wao RAS Simiyu ambapo katika kipindi cha kwanza mcheza aliyevalia
jezi yenye namba 11 Erick Mfugale aliwapatia goli la kuongoza kwa kipindi cha
kwanza hadi mapumziko.
Kipindi cha pili
kilinza kwa timu zote kusaka ushindi ili kujihakikishia hatua inayofuata.
Dakika ya saba ya
kipindi cha pili mchezaji aliyevalia jezi namba 8 Maurus Ndenda ndiye
aliwanyanyua mashabiki wa timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo kwa kufunga goli la pili kwa shuti kali na kuingia wavuni.
Hadi kipenga cha mwisho
cha mwamuzi wa mchezo huo Ramadhani Omari, timu ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo imeshinda 2 na RAS Simiyu hawajapata kitu ambapo ubao wa
matokeo ulisomeka (Habari 2-Simiyu 0).
Aidha kwa upande wa
mpira wa pete timu ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo bahati
haikuwa yao wamefungwa goli 39 kwa 10 na wapinzani wao Wizara ya Ardhi, Nyumba
Na Maendeleo ya Makazi.





No comments:
Post a Comment