Barabara ya Tegeta itakayozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete kesho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za
ufunguzi wa barabara ya Mwenge- Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba 2014.
Ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye
urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la
Lugalo njia panda ya Kawe.
Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni
sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari
katika jiji la Dar es Salaam.
Taarifa hii imetolewa na;
Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini(GCU)
Wizara
ya Ujenzi


No comments:
Post a Comment