TANGAZO


Tuesday, September 30, 2014

Kinana awataka viongozi waliosababisha Kiwanda cha Chai cha Mponde, Bumbuli, wilayani Lushoto wawajibike ama wawajibishwe


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwapungia wananchi mikono alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mponde, Jimbo la Bunbuli, ambapo aliwahakikishia wananchi kulitafutia ufumbuzi tatizo la kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde, wilayani Lushoto, mkoani Tanga. Kinana aliwataka viongozi wote wa CCM na Serikali waliohusika kufungwa kwa kiwanda hicho na kuwasababishia adha wananchi kuwajibika wenyewe au kuwajibishwa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mponde.
 Kinana akihutubia katika mkutano huo.
Kinana akikagua shamba la chai lililoachwa kutunzwa baada ya kiwanda cha chai cha Mponde kufungwa tangu mwaka jana.
Kinana (kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba na Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Lushoto, Balozi Abdi Mshangama wakiangalia jinsi chai ilivyoharibika baada ya kiwanda kufungwa.
Diwani wa Kata ya Guga, Richard Mbughuni akitolewa na askari baada ya wananchi wa Bumbuli kumwambia Kinana amtoe katika mkutano huo, wa hadhara, wakidai ndiye mmoja wapo wa waliosababisha kiwanda hicho, kifungwa mwaka jana.
Diwani wa Kata ya Guga, Richard Mbughuni akitolewa na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye baada ya wananchi wa Bumbuli kumwambia Kinana aondoke katika mkutano huo wa hadhara, wakidai ndiye mmoja wapo wa waliosababisha kiwanda hicho, kifungwa mwaka jana.
 Wananchi wakishangilia wakati Kinana akiwasili kwenye mkutano huo.
 Kinana akijadiliana jambo na Nape pamoja na January Makamba, Mbunge wa jimbo hilo, la Bumbuli.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, Jamuary Makamba, akihutubia katika mkutano wa hadhara na kumuomba Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana asaidie kutafuta suluhu ya kufungwa kwa kiwanda hicho.
January Makamba akihutubia katika mkutano huo, ambapo aliwaomba msamaha wanachi kwa kuendelea kuteseka kwa kufungwa kiwanda hicho.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji kuhusu mgogoro wa kufungwa kwa kiwanda hicho muhimu.
 Kinana akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika mkutano huo.
Makamba akielezea historia ya jengo la Chama katika Kijiji cha Mbuzii lililokuwa linatumiwa na viongozi wa TANU enzi za ukoloni wakati wakiwa katika harakati ya kutaka kuanzisha chama hicho na uhuru wa Tanganyika.
 Kinana akihutubia kabla ya kushiriki ujenzi wa Kata ya Mbuzii, Lushoto Tanga.
Kinana akishiriki ujenzi wa jengo la CCM, tawi la Mbuzii huku akisaidiwa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba.
Kinana na Makamba wakikagua jengo hilo, la zamani linalokarabatiwa na wananchama wa chama hicho.
 Kinana akimkabidhi nyaraka Kiongozi wa  waendesha pikipiki  ikiwa ni ishara yakuzindua umoja huo.
Nape akiwa amepanda pikipiki katika Mji wa Bumbuli
Kinana akimwangalia Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba akiwa amepakiwa kwenye pikipiki ili awahi kwenye mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, akiendesha pikipiki kuelekea Kata ya Dule ambako Kinana alizindua kikundi cha wajasiriamali cha Maisha Pluis Jimbo la Bumburi, Lushoto.
  Januari Makamba  akimtambulisho Nape.

No comments:

Post a Comment