Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa (kulia) alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl (kushoto) na wandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl akiongea na wajumbe kutoka TAMISEMI na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa Fedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI).
Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl akiongea na wajumbe kutoka TAMISEMI na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa Fedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI).
Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), nchini Judith Karl (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka TAMISEMI na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Mpango wa Fedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI). Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa.
Mtaalamu wa Ushauri wa UNCDF Peter Malika (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu LFI na chini ambapo amesema kuwa lengo lake ni kutoa ushauri wa kitaalamu, fedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija katika jamii ili wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na taifa kwa ujumla. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius Mtasiwa na kushoto ni Afisa Habari TAMISEMI Rebecca Kwandu.(Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na
Eleuteri Mangi – MAELEZO
16/09/2014.
SERIKALI ya Tanzania
itafaidika kwa kupata fedha za maendeleo zaidi ya Sh. 46400 za kitanzania
ambazo ni sawa na dola milioni 29 za kimarekani ili kusaidia miradi mbalimbali
ya maendeleo nchini.
Kati ya fedha hizo,
zaidi ya sh. milioni 41600 za kitanzania ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani
milioni 26 ni mkopo na sh. 4800 za Kitanzania ambazo ni sawa na Dola milioni tatu ni msaada kutoka Shirika
la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na
Mfuko wa Maendeleo (UNCDF) nchini ambazo zinatarajiwa
kunufaisha miradi mitano kwa miezi sita hadi tisa inayokuja.
Ili kufanikisha azma
hiyo, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha
na Mfuko wa Maendeleo ( Capital
Development Fund) wamezindua Mpango wa Kifedha wa Kidunia na Kitaifa (LFI)
ambao utatekelezwa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2014 hadi
2017.
Mradi wa LFI nchini
unasaidia miradi 25 katika sekta za umeme, miundombinu vijijini, mawasiliano,
viwanda na masuala ya usindikaji katika mikoa 10 ambapo mikoa ya Pwani na
Kilimanjaro kupitia halmashauri za Kibaha na Same ni miongoni mwa halmashauri
zinazonufaika na mradi huo.
Kauli hiyo imetolewa na
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu kataka Wizara hiyo Dkt. Deogratius
Mtasiwa alipokuwa katika mkutano na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia masuala ya Fedha za Maendeleo ya Mitaji (UNCDF)
nchini Judith Karl leo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mtasiwa amesema
kuwa Serikali inajukumu la kutoa huduma za jamii kulingana na mazingira ya
ndani ambapo jukumu hili linasimamiwa katika ngazi ya halmashauri wakati
Serikali Kuu jukumu lake ni kupanga na kutoa sera zinazosimamiwa na kutekelezwa
katika ngazi ya Serikali za Mitaa.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Fedha za Maendeleo ya
Mitaji (UNCDF) nchini Judith Karl amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya
Serikali ya Tanzania kupitia TAMISEMI umekuwa ni kiini cha kutekeleza mipango
mbalimbali inayosimamiwa na UN.
Aidha, Judith amesema
kuwa mpango wa LFI unalenga kuongeza uboreshaji wa rasilimali fedha kwa
maendeleo ya kiuchumi kupitia mitaji na masoko ili kuweza kukuza na kufikia
malengo ya maendeleo ya ndani ya nchi.
Naye Mtaalamu wa
Ushauri wa UNCDF Peter Malika amesema lengo la LFI l ni
kutoa ushauri wa kitaalamu, kifedha na namna ya kuchagua miradi yenye tija
katika jamii ili kuwawezesha wananchi waweze kujiletea maendeleo yao wenyewe na
taifa lao.
No comments:
Post a Comment