Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Haak Neel Production, Godfrey Mahendeka (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho ya siku hiyo, itakayoadhimishwa Oktoba 25, mwaka huu, Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya maadhimisho, Suleiman Lingande na katikati ni Abdul Salvador.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Haak Neel Production, Godfrey Mahendeka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho hayo, yatakayofanyika Oktoba 25, mwaka huu, Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya New Habari (2006), wadhamini wa maadhimisho hayo, Michael Budigila na katikati ni Mratibu wa Masoko wa Siku ya Msanii, Catherine Metili.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Haak Neel Production, Godfrey Mahendeka (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuhusu maadhimisho hayo, yatakayofanyika Oktoba 25, mwaka huu, Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Matukio wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Kurwijira Maregesi, Meneja Masoko wa Kampuni ya New Habari (2006), wadhamini wa maadhimisho hayo, Michael Budigila na watatu ni Mratibu wa Masoko wa Siku ya Msanii, Catherine Metili.
Mkuu wa Matukio wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Kurwijira Maregesi (kushoto), akifafanua jambo katika mkutano huo. Wapili ni Meneja Masoko wa Kampuni ya New Habari (2006), wadhamini wa maadhimisho hayo, Michael Budigila,Mratibu wa Masoko wa Siku ya Msanii, Catherine Metili, Meneja Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Haak Neel Production, Godfrey Mahendeka, Wajumbe wa Kamati ya maadhimisho ya Siku ya Msanii, Abdul Salvador na Suleiman Lingande.
Mwandishi wa habari wa Dutch Well (DW), Hawa Bihonga, akiuliza swali kuhusu maadhimisho hayo.
SIKU ya Msanii Tanzania inatarajiwa kuadhimishwa Oktoba 25
mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam.
Hii ni siku ambayo wasanii kutoka katika nyanja mbalimbali
za sanaa wataungana pamoja kuadhimisha siku yao. Lengo mahsusi la siku ya
msanii Mradi huu ulibuniwa ili
kuungana na wenzetu duniani kote kuadhimisha siku ya kimataifa ya Msanii
(International Artist Day) ambayo Kuadhimishwa kila mwaka tarehe 25 Oktoba ili
kumtambua msanii, kazi zake pamoja na mchango wake katika jamii.
Kama ilivyo kwa maadhimisho mengi kama vile Mei Mosi, Siku ya
UKIMWI Duniani, Siku ya Wanawake
Duniani, n.k. Baraza limeona ni
vema kuwepo na Siku ya Msanii ambayo
itaadhimishwa kitaifa kila mwaka Mwezi Oktoba, kilele chake kitafanyika katika
Mikoa mbalimbali kulingana na uwezo wa kifedha kwa mwaka husika.
Kauli mbiu ya siku ya Msanii 2014 ni “Sanaa ni Kazi”. Fani zifuatazo ndizo zinazotarajiwa kutumika katika tukio
hili; taarabu, muziki wa dansi, ngoma za asili, muziki wa msanii kutoka nje ya
nchi, uchezaji shoo, dansi za mitaani, Bongo fleva, maonyesho ya mitindo ya
mavazi, semina, sanaa kwa watoto na maonyesho ya sanaa za ufundi.
Katika kuadhimisha siku hii kutakuwepo na shughuli
mbalimbali za sanaa ikiwepo utoaji wa Tuzo. Tuzo zitakazotolewa ni pamoja na
Tuzo ya Msanii aliyejitolea maisha yake yote katika maendeleo ya Sanaa (Life Time Achievement Award) na Tuzo ya
Msanii aliyetoa mchango mkubwa katika jamii kupitia sanaa (Humanitarian Award) kwa kuanzia. Tuzo hizi zitatolewa kwa wasanii
raia wa Tanzania pekee (walio hai au waliokwishafariki dunia) ambao wamefanya
kazi za sanaa katika kipindi cha kuanzia mwaka 1964 hadi 2013.
Mchakato wa utoaji fomu za Tuzo hizi utaanza tarehe 15
Septemba mpaka tarehe 3 Oktoba 2014
ambapo wasanii,jamii na wadau wa sanaa watajaza fomu ili kupendekeza majina ya
wasanii wanaostahili kupewa Tuzo hizi.
Fomu za Tuzo hizi zinapatikana bure katika Ofisi za Haak
Neel Production Ltd Barabara ya Garden, Nyumba Namba 493, Ofisi za Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA), Ilala Sharif Shamba na Ofisi za Mashirikisho ya Sanaa
nchini. Pia wadau wanaweza kupata hizi fomu kupitia tovuti za www.haakneelproduction.com, www.sikuyamsanii.co.tz, magazeti ya
Dimba, Bingwa na Mtanzania, blogu ya Michuzi na mitandao mbalimbali ya kijamii.
Baada ya fomu hizo kujazwa kikamilifu zitarejeshwa kwa njia
ya mkono au kutumwa kwa anwani zifuatazo:
Haak Neel Production (T) Ltd
Mikocheni Garden Road Nyumba namba 493,
S L P 32419 Dar Es Salaam, Barua pepe: info@haakneelproduction.com, info@sikuyamsanii.co.tz
Au
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Ilala Sharif Shamba,
S L P 4779 Dar Es Salaam, Barua pepe: basata06@yahoo.com
Imetolewa Septemba 15, 2014, Dar Es Salaam.
KAMATI YA SYM 2014
Justine K Jones
Mratibu Mkuu
No comments:
Post a Comment