Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mary Meela, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu wajibu na majukumu yake kwa jamii.
Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile. (Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu majukumu ya shirika hilo, jinsi yanavyotekelezwa na Kurugenzi ya Udhibiti Ubora. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mary Meela.
Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mary Meela (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Ofisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Frank Mvungi na Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile.
Na Frank Mvungi-Maelezo
Shirika la viwango Tanzania (TBS) linatarajia kuajiri watumishi 200 katika harakati za kuimarisha utendaji wa shirika hilo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa udhibiti ubora wa shirika hilo Bi Mary Meela wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Akifafanua Meela amesema watumishi watakaoajiriwa watasaidia kuimarisha utendaji kazi wa shirika hilo hasa katika kufanya ukaguzi na kuhakisha tatizo la bidhaa hafifu linapungua au kuondolewa kabisa.
Aidha Bi. Meela alisema kuwa Shirika limeweza kuweka wakaguzi kwenye vituo 5 ambavyo ni Sirari, Namanga, Taveta, Horohoro, Bandari za Tanga na Dar es salaam na kuweka wakaguzi kwenye vituo vya bandari kavu (ICD).
Akizungumzia kuhusu utumiaji wa nguo za ndani za Mtumba Bi. Meela amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kupinga matumizi ya nguo hizo kwani zina madhara kiafya kwa watumiaji na wataendelea kufanya ukaguzi wa nguo hizo na kuziteketeza pindi zinapopatikana.
Shirika la viwango lilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 3 ya mwaka 1975, kasha kuundwa upya mwaka 2009 sheria ambayo imelipa shirika uwezo mkubwa zaidi wa utayarishaji viwango na kusimamia utekelezaji wake.
No comments:
Post a Comment