Taasisi ya Benjamin Mkapa yakusanya sh. bil. 1.38 Mwanza
Kwa
niaba ya Msarifu wa Taasisi Mhe. Benjamin William Mkapa, Bodi ya Wadhamini,
Menejimenti na wafanyakazi wa Taasisi ya Benjamin William Mkapa tunatoa
shukrani za dhati kwa kuweza kufanikisha harambee ya kuchangia. Mradi wa Mkapa
Fellows, iliyofanyika jijini Mwanza siku ya Jumamosi, tarehe 23 Agosti 2014
katika ukumbi wa Hotel ya JB Belmont.
Harambee
iliyohudhuriwa na wageni karibia 230 iliongozwa na Waziri Mkuu wa Tanzania,Mhe Mizengo
Pinda ambae alikuwa mgeni rasmi akiambatana na Raisi mstaafu,Mhe. Benjamin W.
Mkapa pamoja na Mama Anna Mkapa.
Harambee
hii iliyofanyika na Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ni ya mara ya kwanza kutekelezwa
na Taasisi nje ya Mkoa wa Dar Es Salaam. Kwa hatua za awali tuliamua kuanzia katika
Kanda ya Ziwa,na kuwashirikisha washikadau waliopo katika mikoa sita (6) ya
Kanda ya Ziwa. Harambee ilifanikiwa kukusanya kiasi cha Tshs 1.38billioni na hivyo
kuvuka lengo lililowekwa la kukusanya kiasi cha Tsh 500 millioni katika Kanda
hiyo.
Kiasi
kilichokusanywa kitatumika kutekeleza mradi wa Mkapa Fellows unaoendeshwa na Taasisi
ya Benjamin W. Mkapa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania. Mradi huu wa
Mkapa Fellows unatekelezwa katika mizunguko miwili; ambapo mzunguko wa kwanza
ulianza Januari 2013 na utamalizika Desemba 2014 na ulifikia Halmashauri sita
(6) nchini za Sumbawanga vijijini, Kalambo, Nkasi, Msalala, Kishapu na Biharamulo.
Baadhi ya mafanikio ya mradi huu hadi leo, ni pamoja na tumeshaajiri na kuwapeleka
katika wilaya hizo 6 wataalam wa afya 30 kati ya lengo la miaka mitano la
watalaam 180, na pia ujenzi wa vyumba vya upasuaji 9 kati ya 30 umeshakamilika,
na ununuzi na uwekaji wa vifaa vya kutolea huduma pia kukamilika. Fedha za utekelezaji
wa mzunguko huu wa kwanza zilifanikiwa kupatikana kupitia mfadhili wa Serikali ya
Ireland na wafanyabiashara zaidi ya 50, wakiwemo pia Kampuni ya African Barrick
Gold.
Mzunguko
wa pili wa huu mradi utaanza Januari 2015 mpaka Desemba 2017 na utafikia Halmashauri
9 za Shinyanga vijijini, Kahama,Meatu, Bariadi, Itilima, Busega, Maswa,,Chake
Pemba na Mkoa wa Kati Unguja.
Kwa
muhtasari fedha hizi zilizokusanywa katika Harambee hii ya Kanda ya Ziwa,zitasaidia
kuchangia katika bajeti inayohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi kuanziaJanuari
2015. Hali kadhalika mradi wa Fellows ambao una bajeti ya Tshs. 15bilioni kwa miaka 15, ilikuwa bado na pengo la Tshs.
10billion, hivyo kwa kupata mchango wa kutoka Kanda ya Ziwa wa Tshs. 1.3billioni,sasa
litapunguza hilo pengo hadi Tshs. 8.7 bilioni. Wakati huo huoTaasisi itaendelea
na mikakati mingine mbalimbali ya kutafuta fedha za kutekeleza mradi huu hadi mwaka
2017.
Kwa
nafasi ya pekee, Taasisi ya Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS (BMAF) inapenda kutoa shukrani
zake kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda kwa kukubali mwaliko wa kuwa
mgenirasmi katika harambee hiyo. Pia shukrani zinatolewa kwa mawaziri na manaibu
mawaziri na viongozi mbalimbali ambao walituunga mkono katika Harambee hii.
Taasisi
inatoa shukrani zake kwa Wakuu wa mikoa wa Kanda ya Ziwa kwa kukubali kwao kuongoza
mikoa na Halmashauri zilizopo chini yao, katika maandalizi na kushiriki kikamilifu
katika harambee hii. Aidha Taasisi ya BMAF inatoa shukrani za dhati kwa wafanyabiashara
wote wa Kanda ya Ziwa kwa kuweza kuchangia katika mradi huu. Mafanikio haya ni mfano
mzuri wa Public-Private Partnership (ushirikiano kati ya sekta binafsi na sekta
ya umma/serikali), ambapo inaweza kuleta mabadiliko katika kuimarisha huduma za
afya nchini. Moyo na uaminifu waliotuonyesha ni mkubwa na tuna Imani
tutaendelea kushirikiana katika kuleta maendeleo ya sekta ya afya, hususan katika
maeneo ya vijijini.
Shukrani
za pekee ziwaendee wadhamini wetu waliofadhili hafla ya chakula cha jioni cha
harambee, ambao ni Anglo-Gold Ashanti, NSSF, Bank M, PPF,NHIF, Nyanza Bottling
Co, Montage Limited, JB Belmont, Afya Radio,Mwananchi Communication, Jembe ni Jembe,
Isamilo Hotel, Clouds FM naSahara Media Group.
Imetolewa
na:
Dkt
Ellen Mkondya-Senkoro
Afisa
Mtendaji Mkuu
Taasisi
ya Benjamin William Mkapa
S.
L. P 76274, Dar es Salaam
Tarehe: 10 Septemba 2014
No comments:
Post a Comment