Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani
ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu
ya Katiba.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani
ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu
ya Katiba.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani
ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu
ya Katiba.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani
ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu
ya Katiba.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani
ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu
ya Katiba.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiingia ndani
ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa Rasimu
ya Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta
akitoa maelezo muhimu wakati wa mjadala wa Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014
Bungeni mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta
akitoa maelezo muhimu wakati wa mjadala wa Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014
Bungeni mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba toka Kamati namba Tano, Mhe.
Asha-Rose Migiro (kushoto) akiwa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Frederick Werema wakifuatilia mjadala wa Bunge hilo 10 Septemba, 2014 Bungeni
mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samia
Suluhu Hassan (kushoto) akiwa pamoja na mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Pandu Ameir
Kificho wakifuatilia mjadala wa Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 Bungeni mjini
Dodoma.
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru (kushoto) akiwa na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
Mhe. Margareth Sitta wakifuatilia mjadala ndani ya Bunge hilo leo 10 Septemba,
2014 Bungeni mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Angellah Kairuki
(kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Watanzania waishio Marekani, Mhe. Kadari Singo
wakifuatilia mjadala ndani ya Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 Bungeni mjini
Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiendelea
kufuatilia mjadala wa Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiendelea
kufuatilia mjadala wa Bunge hilo leo 10 Septemba, 2014 Bungeni mjini Dodoma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa
kwanza kulia) akiwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalum la Katiba.
Kushoto ni Mhe. Pandu Ameir Kificho na katikati ni Mhe. Seif Khatibu. (Picha zote na Benedict Liwenga,
Maelezo-Dodoma)
Na Benedict
Liwenga, Maelezo-Dodoma
10/09/2014
BUNGE Maalum la Katiba leo tarehe 10
Septemba, 2014 limeendelea na kazi yake ya kusoma na kujadili taarifa za Kamati
mbalimbali Bungeni mjini Dodoma.
Baadhi ya mambo yaliyojadiliwa katika Bunge
hilo ni pamoja masuala ya migogoro ya ardhi inayowahusisha wafugaji na
wakulima, mambo ya Uraia pacha, haki ya afya, haki ya kuishi ikiwemo sheria ya
kunyonga, haki za binadamu, haki ya Mtuhumiwa na Mfungwa, haki za wafanyakazi
na ajira pamoja umri katika ajira pamoja haki za vijana.
Akizungumza wakati wa mjadala huo, Mjumbe wa
Kamati namba Sita, Mhe. Zaina Madabida amesema kuwa ni vema kuwepo kwa
kipengele kinachotambua mila na desturi za makundi ya wafugaji na wakulima ili
kuondoa migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara hapa nchini.
Kuhusu masuala ya Uraia, Mhe. Madabida
ameeleza kuwa si vema kumtambua mtoto mwenye miaka Saba kama raia Mtanzania
aliyekanyaga katika ardhi ya Tanzania na badala yake ni vema mtoto mchanga
ndiyo atambulike kama raia halisi wa Tanzania kikatiba kama Mtanzania, hivyo
yeye na Kamati yake wamekubaliana kumtambua mtoto mchanga kama Mtanzania halisi
ambaye atakuwa amekanyaga katika ardhi ya hiyo.
“Mtoto ambaye ni raia halisi wa Tanzania atakayekutwa
katika ardhi ya Tanzania itambulike kuwa ni yule mtoto mchanga na sio yule
mwenye umri wa miaka Saba”, alisema Mhe. Madabida.
Aidha, Mhe. Madabida amegusia suala la Sheria
ya Haki ya kuishi pamoja na Sheria ya kunyonga akisema kuwa Sheria hiyo ya
kunyonga ni vema iendelee kuwepo katika Katiba kwani kuna watu ambao wao wanaua
wenzao.
“Adhabu ya kifo iendelee kuwepo kama Katiba
yetu ya sasa inavyosema kwani kuna watu wao wamekuwa wakiwaua wenzao”, alisema
Mhe. Madabida.
Kwa upande mwingine, mjumbe toka kamati namba
Tisa amezungumzia kuhusu suala la haki za binadamu akitaja Ibara ya 24 katika
Sura ya Nne, nae amesema kuwa maoni ya wachache yamefafanua kuwa haki ya kuishi
ianzie tangu pale mimba inapotungwa kwani sikuhizi watu wengi wamekuwa na
utaalamu sana katika kutambua viumbe vilivyopo tumboni, hivyo watu hao wamekuwa
wakikatiza uhai wa viumbe wasiokuwa na hatia.
Mjumbe ameongeza kuwa katika Ibara ya 39
inayohusu haki ya Mtuhumiwa na Mfungwa, yeye na kamati yake wameitaka Katiba
izingatie mazingira rafiki kwa watuhumiwa wenye ulemavu na izingatie kuhusu
suala la miundombinu kwa walemavu hao ili iwe rafiki kwani Magereza mengi nchini
yalijengwa kipindi kirefu.
Naye mjumbe wa kamati namba Kumi, Mhe. Monica
Sophu amezungumzia kuhusu suala la ardhi akisema kuwa katika mambo
yanayohusiana na masuala ya ardhi, ni vema ikaundwa Tume Huru ya Ardhi ambayo
itakuwa ina kazi ya kushughulikia masuala hayo ili kuepusha migogoro
inayojitokeza baina ya makundi mbalimbali.
“Katika kutatua suala la migogoro ya ardhi
kati ya wakulima na wafugaji, ni vema kukawepo na Tume Huru ya Ardhi
itakayoshughulikia masuala hayo, hivyo Katiba iwatendee haki makundi haya”,
alisema Mhe. Sophu.
Naye mjumbe wa Kundi la 201, Mhe. Jesca
Msavatavangu amezungumzia juu ya haki za Vijana nchini akisema kuwa, haki hizo za
vijana hazijaainishwa vema, hivyo ameshauri kuwa ni vema sasa Katiba ikaainisha
vema haki hizo ikiwemo kuelezea juu ya ushiriki wao katika nafasi za uongozi
pamoja na kupewa fursa kushiriki katika mambo ya kiuchumi.
“Serikali iweke namna ya kuwaelimisha vijana
wetu kuhusu kazi ili wawe na ujasiri na wajengewe uwezo, pia vijana wapewe
fursa ili waweze kushiriki katika nyanja za kiutamaduni, walindwe dhidi ya afya
na uhai wao”, alisema Mhe. Msavatavangu.
Kuhusiana na suala la Uraia wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Msavatavangu amesema kuwa Sura ya 56 inayohusu suala
la uraia huo ni vema likachukuliwa kwa umakini mkubwa, aidha ameshauri kuwa ni
vema kuwa na uraia wa nchi moja kwani Tanzania bado haijaweza kujilinda
vyakutosha kuweza kukabiliana vitendo viovu vinavyoweza kujitokeza.
“Watu watatumia fursa hii ya Uraia pacha
kuhujumu uchumi wetu, kwani kuna mazingira mengi ya rushwa, hivyo suala la hili
la uraia pacha lije kufikiriwa baadaye sana sio sasahivi”, alisema Mhe.
Msavatavangu.
Naye mjumbe mwingine wa Bunge hilo, Mhe.
Yahya Kassim Issa amegusia kuhusu suala hilo hilo la Uraia pacha akitaja Ibara
ya 38 inayohusu suala la uraia, amesema kuwa kuna watu wenye watoto wao nje ya
nchi na kwa ubinafsi wao ndiyo wanatumia nafasi hiyo kudai uraia huo badala ya
kujali uzalendo na usalama wa nchi yao.
“Haiwezekani kwa mtu uwe na uraia wa nchi
mbili halafu uwe Mwadilifu katika nchi zote hizo mbili”, alisema Mhe. Issa.
Bunge hilo linaendelea na kazi ya kusoma na
kujadili taarifa za kamati mbalimbali kama ilivyopangwa ambapo wajumbe toka
kamati husika wanachangia michango toka katika kamati zao kwa lengo la kujadili
ndani ya Bunge hilo.
No comments:
Post a Comment