Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Baraza la Ushindani (FCT), Nzinyangwa Mchany, akifafanua jambo kwa waandisha, wakati alipokuwa akizungumza kuhusu madai ya aina za rufaa zinazosikilizwa na baraza hilo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Sheria Mwandamizi wa FCT, Hafsa Said. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Baraza la Ushindani (FCT), Nzinyangwa Mchany (hayupo pichani), wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusu madai ya aina za rufaa zinazosikilizwa na baraza hilo.
Wapigapicha wa Televisheni, wakiwa kazini wakati wa mkutano huo na Maofisa wa Baraza la Ushindani nchini jijini leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Baraza la Ushindani (FCT), Nzinyangwa Mchany, akifafanua jambo, wakati alipokuwa akizungumza kuhusu madai ya aina za rufaa zinazosikilizwa na baraza hilo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa Sheria Mwandamizi wa FCT, Hafsa Said.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Baraza la Ushindani (FCT), Nzinyangwa Mchany (hayupo pichani), wakati alipokuwa akifafanua jambo kuhusu madai ya aina za rufaa zinazosikilizwa na baraza hilo. |
Na
Hassan Silayo-MAELEZO
Baraza
la ushindani limewataka wananchi kulitumia Baraza hili kwa manufaa ya Taifa na
ustawi wa uchumi nchini.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi Nzinyangwa Mchany wakati wa
mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
“Baraza
la ushindani lipo kwa ajili ya watu wote hivyo wananchi hawana budi kulitumia
kwa manufaa ya Taifa”. Alisema Nzinyangwa.
Aidha,
Nzinyangwa alisema kuwa baraza la ushindani ni chombo maalum cha rufaa za
maamuzi au amri za Tume ya Ushindani na mamlaka za udhibiti kwenye sekta za
Miundombinu,huduma za maji na nishati.
Pia
alisema kuwa kesi zinazosikilizwa kwenye baraza zinahakikisha uzingatiaji wa
misingi ya udhibiti ili kuleta umakini katika kusimamia sekta husika na
ushindani wa haki sokoni.
Akizungumzia
kuhusu rufaa zilizowahi kusikilizwa na baraza hilo Nzinyangwa alisema kuwa
rufaa zinazosikilizwa na baraza la Ushindani zimegawanyika katika makundi
manne.
Akizitaja
rufaa hizo Nzinyangwa alisema ni rufaa kati ya mtoa huduma na mlaji, hii ni
pale mlaji anapopewa huduma mbovu au hafifu kwenye sekta inayosimamiwa na
mdhibiti kama maji, simu, nishati ya umeme pamoja na bidhaa za mafuta ya
nishati.
Pia
kuna aina ya rufaa kati ya wauzaji wawili wa bidhaa ya aina moja ama mbadala
wake kama kampuni za usafirisha au kampuni za simu ambapo shauri hili
litapelekwa kwa mdhibiti wa sekta husika na iwapo upande mmoja hautaridhika na
uamuzi unahaki ya kuombea rufaa uamuzi huo kwenye baraza la ushindani.
Akiendelea
kutaja Rufaa hizo Nzinyangwa alisema kuwa pia ipo rufaa kati ya mtoa huduma na
mdhibiti wa sekta na hii ni pale mdhibiti wa sekta anapoandaa utaratibu wa
kudhibiti sekta na ikiwa mdau anaona
utaratibu huo hautoshelezi au haukufuata sheria mdau ana haki ya kuwasilisha
malalamiko kwenye chombo kilichotoa uamuzi huo.
Pia
mdau wa soko anaweza kukata rufaa kwenye Baraza la ushindani ikiwa tume ya
ushindani imetoa amri kwenye soko au kutunga kanuni Fulani juu ya utaratibu
kuhusu usimamizi wa ushindani kwenye soko ambao mdau anaona uamuzi huo haukuwa
sawa.
Tume ya ushindani ina jukumu la kukataza
uzalishaji na uuzaji wa bidhaa bandia sokoni,katika jukumu hilo maamuzi hayo
yanaweza kukatiwa rufaa na mdau kwenye Baraza la Ushindani
No comments:
Post a Comment