Waandishi wa habari, kutoka vyombo mbalimbali, wakiwa katika mkutano huo, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kutengeza Magari ya Jossekazi Auto Garage, Joseph Mgaya (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Tamasha la Magari la 'Automobile Clinic', lililodhaminiwa na Kampuni ya TSN Group, kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, litakalofanyika Septemba 27 na 28, mwaka huu, viwanja vya Leaders Club jijini. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wambi Lube Oil Distributor, Omar Omar na katikati ni Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Jonathan Mwanayongo.
Waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo, kuhusu Tamasha la Magari la 'Automobile Clinic', lililodhaminiwa na Kampuni ya TSN Group, kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, litakalofanyika Septemba 27 na 28, mwaka huu, viwanja vya Leaders Club jijini.
Waandishi wa habari, wakiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika mkutano huo, wa Tamasha la Magari la 'Automobile Clinic', lililodhaminiwa na Kampuni ya TSN Group, kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, litakalofanyika Septemba 27 na 28, mwaka huu, viwanja vya Leaders Club jijini.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kutengeza Magari ya Jossekazi Auto Garage, Joseph Mgaya, akizungumza na waandishi wa habari, katika mkutano huo, kuhusu Tamasha la Magari la 'Automobile Clinic', lililodhaminiwa na Kampuni ya TSN Group, kupitia kinywaji chake cha Chilly Willy, litakalofanyika Septemba 27 na 28, mwaka huu, viwanja vya Leaders Club jijini. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni Jast Tanzania, Jahu Kessy.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Kutengeza Magari ya Jossekazi Auto Garage, Joseph Mgaya akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo, Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Wambi Lube Oil Distributor, Jonathan Mwanayongo na kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni Jast Tanzania, Jahu Kessy.
Kampuni ya
Jast Tanzania Limited kwa kushirikiana na Jossekazi Auto Garage and General
supplier wameandaa tamasha la kwanza la Magari la aina yake, linalojulikana kwa
jina la Automobile Clinic, ambalo linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili
mfululizo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam.
Tamasha hilo
limelenga katika kutoa huduma ya kitaalamu ya kiufundi kwa wenye magari (Checkup
and Fix) kutoka kwa mafundi stadi ambao wamebobea katika fani ya ufundi wa
makenika katika aina tofauti tofauti za magari.
Akizungumza
na vyombo vya habari, kwenye ukumbi wa habari Maelezo, Joseph Mgaya mmiliki wa
Jossekazi Auto garage amesema tamasha hili lina lengo kuwakutanisha mafundi
stadi na wenye magari, kwa gharama nafuu sana ya shillingi elfu ishirini tu.
Mgaya
alisema huduma hizo ambazo zilipaswa kugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa kwa
wenye magari, kitatolewa kwa bei nafuu ili kwa makusudi tu ya kukutanisha
mafundi hao na wenye magari,.
Alisema
pamoja na Wateja kutengenezewa Air condition na kujaziwa gesi, kufanyiwa
Electronical scan diagnosis, Kuchekiwa Matairi, kuchekiwa Battery, na kupata
ushauri wa kiufundi kuhusu gari zao, pia tamasha hilo litakuwa ni sehemu ya
kukutanisha watu na kupata burudani.
Mgaya
alisema, Mafundi wapatao 50 waliobobea katika fani ya ufundi magari, wamepatikana
baada ya kufanyiwa usaili wa kina na kupitia mchujo na semina elekezi ili
kuweza kuhudumia magari yanayokadiriwa kufika zaidi ya 6000 kwa siku hizo
mbili.
Pamoja na
hayo, Mgaya alisema “ Tumeandaa warsha maalum kwa kina dada, tunatambua kuwa
asilimia kubwa ya waendesha magari barabarani hivi sasa ni kina dada, tunataka
waelewe ni nini cha kufanya pindi atakapopatwa na hitilafu kwenye gari
mabarabarani. “
Elimu hii
ambayo wameiita ‘Auto First Aid’, alisema itasaidia kupunguza uharibifu zaidi
kwenye magari yao, alisema wakati
mwingine kwenye deshboord ya gari kuna kuwa na alama za hatari, lakini kwa kuwa
gari inatembea wanawake wengi wamekua wakipuuzia alama hizo na matokeo yake wanasababisha
hasara kubwa zaidi.
“Pamoja na
kuwafundisha alama za hatari na nini cha kufanya pindi waonapo alama hizo pia Tutawafundisha
kubadilisha matairi, na nini chakufanya na kuwa nacho ikitokea gari limewaharibikia
njiani. “ alisema Mgaya.
Mgaya ambaye
amefanikiwa sana katika ufundi wa AC za magari, Ndege, na Meli, aliongeza kuwa
fani ya ufundi makenika ni kazi ya kuheshimika kama zilivyo kazi nyingine, na
kuongeza kuwa anaiona fursa kubwa kwa vijana wanaomaliza elimu ya juu.
“Siku hizi
magari yote kuanzia Mwaka 2005 kwenda juu yanatumia vifaa maalum vya computer
na internet, pamoja na kuwa maelezo yanakuja kwa lugha ya kingereza, ufundi
spana wa kurithishwa hivi sasa hauna nafasi,”alisema.
“Tofauti na
zamani ukifeli form 4, unapelekwa kwenye ufundi hali hivi sasa imebadiliilka
fani hii inahitaji wasomi na watu wanaoweza kubadilika na kurudi shuleni kila
mara, kama computer matoleo ya magari kila mwaka yanakuja na vitu tofauti, hivi
sasa break hazina annoying sound, break zikiisha utaona kwenye dashboard,
kutengeneza lazima useme user manual ya kingereza na u download soft ware
kwenye internet,” alisema Mgaya na kusistiza vijana waingie kwenye fani
hii.
Aidha Mkurugenzi
wa Jast Tanzania Limited, Jahu Mohammed Kessy, Mratibu wa Tamasha hilo walisema
kuwa, Automobile Clinic litakuwa zaidi ya Tamasha.
“Katika
kuhakikisha tunautumia muda wa wateja wetu vizuri, wakati gari inafanyiwa
ufundi, kutakuwa na huduma nyingine za ziada zitakazo patikana siku hizo mbili,
kutakuwa na vinywaji, vyakula kama nyama choma, na michezo ya watoto, kutakuwa
na huduma ya kulipia ya kuoshewa magari, kusafishiwa taa, na baadhi ya vifaa
kama Fire extinguisher, manukato ya gari, Triangle na kadhalika vitauzwa hapo
uwanjani,”
Jahu alisema
Tiketi zitauza kabla, na kwamba tiketi hizo zitakuwa katika mfano wa sticker ya
kubandika kwenye magari, na zitapatikana katika vituo vyote vya kuweka mafuta
vya TSN, Supermarket zote za TSN, Kwenye ofisi za Millembe insurance, Bon to
shine, BM hair cutting salon, na Mlimani City.
“Hakutakuwa
na Kiingilio kwa watu, lakini badala yake kwa magari, magari yenye sticker
pekee ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia na kupata huduma hizo, tunashauri wenye
kununua sticker wafike mapema kwani watakao fika kwanza ndio watakao hudumiwa,”
Jahu alisema
katika kurudisha kwa jamamii, mafundi hao hamsini baada ya Tamasha watatembelea
kwenye hospitali ya CCBRT kusaidia wakina mama wenye matatizo ya fistula.
Tamasha hilo
limedhaminiwa na Milembe insurance, Wambi lube oil distributor, TSN, Binslum
tires company Limited, I view, Cocacola, Dreams Limited, Hugo Domingo, Olduvai
Bay Wash, 0-60 autogarage, Meku Auto spear part, Dick Sound, Brand Tiger,
Clouds FM, Auto Beats, Neh Catering, Pamoja na Lim Painting and decorating.
No comments:
Post a Comment