TANGAZO


Thursday, August 28, 2014

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira atoa wito kwa wananchi

Waziri wa  Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt  Binilith akizunguza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam kuhusu mkutano  wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa Nchi za Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 29, 2014 nchini.
Mkurugenzi  Msaidizi wa   Idara ya Mazingira  Suzi Salula akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu mabadiliko ya tabianchi leo jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano  wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa Nchi za Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 29, 2014 nchini.

Lorietha Laurence -Maelezo
WAZIRI wa  Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Binilith Mahenge ametoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za serikali na za Bara la Afrika  kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi ili kupata maendeleo endelevu.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa Nchi za Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 29, 2014.

Mkutano huu wenye lengo la kujadili na kupendekeza masuala muhimu  ya bara la Afrika  kuhusu upatikanaji wa fedha na teknolojia katika kukachangamoto hizo zinazo athiri sekta ya kilimo, usafirishaji, afya, nishati,mifugo,uvuvi,viwanda na maji.
“ni jukumu letu sote kuhakikisha tunakabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutumia gesi na majiko maalum ili kupunguza gesijoto inayopelekea mabadiliko ya tabia ya nchi” alisema Dkt. Mahenge
Aidha aliongeza kuwa  mkutano huo  ni maandalizi ya mkutano unaotarajiwa kufanyika Septembe  23, 2014 ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na ule wa 20 wa Nchi wananchama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Mjini Lima, nchini Peru  Desemba 1-12,2014.  

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa  Idara ya Mazingira Suzi Salula aliongezea kuwa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinahitajika kutiliwa mkazo ili kuweza kujikwamua kuondokana na changamoto hii.
Ripoti ya Wataalamu wa Kimataifa  kuhusu mabadiliko ya tabianchi inaonyesha  kuwa mwaka 2013 joto la dunia limeongezeka kwa nyuzi joto 0.85 juu ya wastani wa joto la dunia na kupelekea ongezeko la gesijoto  na kuathiri  kwa kiasi kikubwa sekta ya Kilimo, nishati, afya, usafirishaji, mifugo, uvuvi, viwanda na maji.

No comments:

Post a Comment