TANGAZO

Friday, August 29, 2014

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Peter Pinda afungua Mkutano

Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Uchumi Vijijini na Kilimo, Roda Tumusiime akizungumza na wajumbe ambao ni Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, jijini Dar es Salaam, kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi za Afrika.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda, ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika akisoma risala ya ufunguzi wa mkutano huo, jijini Dar es Salaam, wenye lengo la kupata muongozo wa kujadili changamoto za mabadiliko ya tabia nchi kwa nchi za Afrika ili kuwasilisha maazimio hayo katika mkutano unaotarajiwa kufanyika Septemba 23, 2014 nchini Marekani.

Waziri wa Maji na Mazingira wa Uganda, Eprahim Kamuntu akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi leo, jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku moja wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika.
Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (katikati), ambaye pia ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika, akifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Kamishna wa Umoja wa Afrika anayeshughulikia Uchumi wa Vijijini na Kilimo Roda Tumusiime na kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dkt. Bilinilith Mahenge.
Wajumbe wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda (wapili kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda (wapili kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya Nje kutoka Nchi za kamati ya Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la  kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi kwa nchi hizo, leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)

No comments:

Post a Comment