TANGAZO


Friday, August 29, 2014

Tanzania yagundua Gesi asilia yenye ujazo wa cubic mita trilioni 50.5


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo limejumuisha wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa.

Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa mikoa ya Mbeya Abbas Kandoro (katikati) na Lindi Ludovick Mwananzila( kushoto) na Mjiolojia Mwandamizi kutoka Idara ya Nishati Adam Zuberi (kulia) wakisikiliza  mada ya  rasimu ya sera ya Petrol iliyokuwa inatolewa leo katika kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu hiyo lililofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Nishati Eng. Hosea Mbise akiwasilisha  mada kuhusu rasimu ya sera ya Petroli kwa wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na  mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa  wakati wa kongamano la kupata maoni ya wadau linalofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.


Kamishna wa Nishati Eng. Hosea Mbise (kushoto) akimpongeza  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro mara baada ya kufungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na  mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa mafuta na gesi, wabunge, viongozi wa dini na  mikoa iliyofanyiwa utafiti wa mafuta na gesi  na vyama vya siasa wakimsikiliza  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika jijini Dar es Salaam.


Waandishi wa mkutano  (Rapporteur)  wakiandika  taarifa mbalimbali wakati wa  kongamano la  siku moja la kupata maoni ya wadau  kuhusu rasimu ya sera ya Petroli linayofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Anna Nkinda- Maelezo)


Na Anitha Jonas – Maelezo
TANZANIA imegundua gesi asilia katika maeneo 19  ya mwambao na kina kirefu cha maji baharini ambayo ina ujazo wa trilioni 50.5.
Kati ya maeneo hayo  19 yaligundulika gesi  hiyo ,matano yanapatikana katika mwambao na 14 yapo katika kina kirefu cha maji baharini .
Hata hivyo gesi iliyogundulika katika maeneo ya mwambao kama Songo songo na Mnazi Bay kwa sasa inatumika kufua umeme na pia kwa ajili ya matumizi ya viwandani,majumbani na kwenye magari.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa   Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro  wakati akifungua kongamano la wadau wa mafuta na gesi linalofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa huyo amewataka wadau hao watumie muda wao kutoa maoni yatakayosaidia kuwa Sera ya Mafuta na Gesi asilia itakayowanufaisha watanzania pindi itakapoanza kutumika.

Kandoro ameongeza kuwa ni vema Sera hiyo ikasaidia Serikali kupata mapato yake yatakayotokana na Mafuta na Gesi asilia kwa ajili ya kuleata maendeleo mbalimbali kwa manufaa ya wananchi wake.
“Uandaaji wa sera hii ulipitia marejeo ya  nyaraka mbalimbali  ikiwemo sera ya petroli za nchi zilizogundua nishati ya  mafuta na gesi asilia zikiwemo Uganda,Ghana,Sierra Leone na Pakistani”.

Mpaka Oktoba mwaka jana (2013) Serikali ilikuwa imekamilisha sera ya gesi asilia ,hii ni kwa ajili ya kutoa muongozo wa kusimamia na kuendesha biashara ya gesi  asilia katika uchakataji,usafirishaji  na usambazaji”, alisema Kandoro.

Amesema  kuwa  Sera hiyo itazingatia na kuangalia kwa ukaribu suala la udhibiti wa mazingira ukomo wa uzalishaji wa rasilimali hiyo pale utakapoanza.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Jiolojia kutoka  Wizara ya Nishati na Madini Adam  Zuberi amesema lengo la sera hiyo ni kuhakikisha rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha watanzania wote kwa  mapato yatakayopatikana katika maeneo husika  kwani asilimia 3 itabaki Halmashauri kwa  matumizi ya wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba  ameishauri Serikali kuwa makini katika makubaliano na makampuni yatakayochimba gesi katika mgawanyo wa mapato kama inavyoonyesha katika sera kuwa asilimia 60 ya mapato itapelekwa  Serikalini. Pia  umakini na uangalifu wa hali ya juu unahitajika kwenye makubaliano hayo.

Mkutano huo wa wa siku moja uliandaliwa na wizara ya Nishati na Madini na kujumuisha  wataalam mbalimbali waliobobea katika masuala ya mafuta ,wawakilishi wa ofisi za ubalozi zilizopo nchini ,Vyama vya siasa , viongozi wa dini, Wakuu wa Mikoa  na asasi za kiraia.

No comments:

Post a Comment