Na Winner Abraham-MAELEZO-Dar es salaam
UONGOZI
wa ZION SOUNDS umeandaa tamasha la kuelimisha jamii kuhusu
athari za dawa ya kulevya linatarajia
kufanyika mapema mwezi ujao.
Tamko hilo limetolewa na Mtendaji Mkuu wa ZION
SOUNDS Bw. Junior Zion wakati wa mkutano
na waaandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa wameamua kuandaa tamasha hilo ili
liweze kuwaelimisha vijana kuacha kujiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya.
“Kama tunavyojua kuwa vijana ndio viongozi wa baadaye
hivyo wanahitaji msaada mkubwa katika makuzi na kuelimishwa ni jinsi gani
wataepukana na janga hili hivyo wahamasishwe kwa njia tofauti tofauti”amesema
Zion.
Ameongeza kuwa kwa takwimu za nyuma kidogo karibu ya
asilimia 40% ya vijana tayari wanatumia dawa za kulevya kama Cocaine na bangi.
Naye Meneja Matukio wa Zion Sounds Bi.Careen
Dora Bi Careen ametaja sababu
zinazochangia vijana wengi kujiingiza
katika matumizi ya dawa na pombe kuwa ni
kama kutaka kujua kwani kipindi cha ujana ni kipindi ambacho wengi hutaka kujua
vitu vingi ambavyo ni vigeni kwao.
Amesema kuwa vijana wanaoanza kutumia pombe wakiwa
na umri wa miaka 15 wanaathirika mara 5 zaidi wanapofikia umri mkubwa.

No comments:
Post a Comment