TANGAZO


Monday, August 11, 2014

Shirika la YMC laendesha mafunzo ya siku kumi kwa vijana Mjini Singida


Maratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la YMC, Fidelis Yunde, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa vijana ya siku kumi kwenye viwanja vya Mandewa mjini Singida jana

Na Hillary Shoo, 
Singida.
SHIRIKA lisilo la kiserikali ya YMC limetoa elimu ya masuala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa jumla ya vijana 40,000 wenye umri kati ya miaka 15 na 24 katika Halmashauri nne za Mkoa wa Singida kwa kipindi cha miaka mitatu.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kufunga mafunzo kwa vijana ya siku kumi jana kwenye viwanja vya Mandewa mjini hapa Maratibu wa shirika hilo Fidelis Yunde alisema katika kipindi hicho juma ya vilabu 186 viliundwa kwa ajili ya ujasiriamali.


Yunde alisema vuijana hao wamepewa mafunzo ya kufikisha ujumbe mbalimbali kwa jamii juu ya masuala ya afya ya uzazi na ujinsia kwa kutumia mbinu mbalimbalia akama vile vikaragosi, ngoma, maigizo na sanaa.
Aidha alisema shirika lake linatekeleza mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na ujinsia wa TMEP unaotekelezwa na shirika la HAPA chini ya ufadhili wa shirika la USAID chini ya Wizara ya afya na ustawi wa jamii.

Alisema katika kipindi hicho cha utekelezaji wa mradi huo wa TMEP ambao unaenda ukingoni kati ya vilabu 186 wameweza kusajili vikundi 26 kama SACCOS kwa kupata usajili wa kudumu kama vikundi halali vya ujasiriamali.

Alisema YMC imeongeza wigo kwa vijana kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na matatizo mbalimbali ikiwemo kupata mimba za utotoni , madawa ya kulevya na utoro mashuleni.

Akifunga mafunzo hayo Mratibu wa kudhibiti maambukizi ya Ukimwi Mkoa wa Singida (TACAIDS), Mdala Fedes, alisema kujifunza kwa kuangalia inaelimisha jamii vizuri zaidi.

Aliwataka vijana kuendelea na kufikisha jumbe hizo, ili kupunguza kupungza watoto wa mitaani ambao wengi wao wanazakliwa katrika mazingira magumu.
Fedes pia aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao vizuri katika kuelimisha jamii juu ya masuala ya uzazi na ujinsia.

Hata hivyo alisema kwa kutumia njia ya vikaragosi mwitikio wa wanaume umeongezeka kutoka wastani wa wanaume watano hadi hamsini katika kipindi hicho kuhudhuria kliniki pamoja na wenza wao.

No comments:

Post a Comment