TANGAZO


Monday, August 11, 2014

Liverpool imeilaza Dortmund 4-0


Liverpool inajianda kwa msimu mpya wa ligi ya Uingereza

Mshambulizi wa Liverpool Dejan Lovren aliifungia the Reds bao lake la kwanza katika mechi yake ya kwanza Liverpool ilipoilaza Borussia Dortmund mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki.
Daniel Sturridge ndiye aliyeifungua kivuno hicho cha mabao baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Phillippe Coutinho.
Lovren, aliyejiunga na ''the Reds'' akitokea Southampton, katika kandarasi ya pauni milioni 20m alifuma bao la pili kwa kichwa alipotumia vyema kona kutoka kwa Steven Gerrard.


Liverpool inajianda kwa msimu mpya wa ligi ya Uingereza
Jordan Henderson alikamilisha kivuno hicho baada ya kufaidi pasi ya Sturridge.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers aliwachezesha wachezaji wapya Lovren, Javier Manquillo, Emre Can, Rickie Lambert katika mechi hiyo.
Liverpool, itafungua kampeini ya msimu huu dhidi ya Southampton jumapili ijayo.


Kocha Rodgers aliwachezesha wachezaji wapya
Kwa upande wao Dortmund ilikuwa inatumia mechi hiyo kujiandaa kwa mechi dhidi ya Bayern Munich ya kuwania kombe la German Super Cup siku ya jumatano.
Dortmund itafungua kampeini yake dhidi ya Bayer Leverkusen tarehe 23 Agosti.

No comments:

Post a Comment